Ads

Amana banki yaanza ukusanyaji wa zakat ili kuisaidia jamii





Na Rayusa Yasini
 mwamba wa habari
WAISLAM nchini wameombwa kutimiza nguzo yao ya Tatu kwa kutoa zakat baada ya benki ya Amana nchini kupewa idhini hiyo ya ukusanyaji na ugawaji zakat kwa jamii isiyojiweza.

Wito huo umetolewa Leo jijini Dar yes salaam na mkurugenzi mtendaji Muhsini Masoud wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo kutokana na mahitaji makubwa katika jamii. 

    Amesema baada ya kuidhinishwa na benki kuu kuwa chombo makini chenye kuratibu vizuri ukusanyaji na ugawaji wa zakat waislam watimize wajibu wao kwa urahisi .

"Tunatoa huduma hii kwa uwazi na kwa utaratibu ulio bora chini ya muongozo makini wa bodi ya usimamizi wa sheria na tutazigawa kwa wanaostahiki kama walivobainishwa kwenye kur'an"

Amesema watakaopewa sadaka hizo baada ya ukusanyaji ni mafakiri' na masikini' na wanaozitumikia na wakutiwa nguvu nyoyo zao katika kukomboa watumwa pamoja na wenye madeni.

Kwa upande wake naibu katibu mkuu wa baraza la sunna shehe Mohammed Issa amewaomba waislam na kuchangamkia utoaji wa zakat kwa kuwa wamejipanga ili ziweze kuwafikia 

walengwa.
"TUtawasaidia wateja wetu kuwafikia wale wanaostahiki zaidi waweze kupata pamoja na kutembelea tovuti ya benki (WWW.amanabenki.co.tz./sw/akaunti-ya-akiba-binafsi.

Benki ya amana inaendesha zoezi la upokeaji zakat kupitia wateja wao ili jamii isiyojiweza iweze kupata zakat hizo kupitia akaunti namba (002110475520001) pamoja na kupitia kwa mawakala wote waliopo nchi nzima huku waislam wakiombwa kuchangamkia fursa hiyo ya utoaji Dhaka.

No comments