BIASHARA YA UJAMBAZI HAILIPI:KAMISHINA SIRRO.
Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kuhusika na matukio mbali mbali ikiwemo ya ujambazi jijini hapa.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kamishina wa polisi kanda maalumu ya dar es salaam,Simon Sirro amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa EUJI ELIAS mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa yombo duvya Temeke baada ya watu wasiojulikana kuvamia kampuni ya Group six na kumjeruhi muhasibu wa kampuni hiyo nakufanikiwa kupora magari mawili;vipande 13 vya meno ya tembo pamoja na mashine ya kukatia vyuma.
Katika hatua nyingine kikosi maalumu cha kupambana na majambazi kimemuua kwa kumpiga risasi mtu mmoja ambaye jina lake halijajulikana katika eneo la masaki jijini humo baada ya kutaka kumvamia mwendesha bajaji na kutaka kumpora , ambapo jehi hilo lililfika katika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata jambazi huyo.
Aidha jeshi hilo limewataka wakazi wa jiji la dar es salaam kuendelea kuwafichua waharifu mbalimbali wakiwemo wanaomiliki silaa kinyume cha sheria ili kuuhakikisha wanapambana na vitendo viovu hapa nchini.
Post a Comment