Ads

SADC kudumisha usalama katika usafiri wa Anga.




SADC  kudumisha usalama katika usafiri wa Anga.
Na Ally Daud-Maelezo
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) imeadhimia kuimarisha  usafiri wa anga ili luleta huduma bora na kuwapa amani  wananchi wanaotumia usafari wa anga katika Jumuiya hiyo.
Hayo yamesemwa  leo na  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Mheshimiwa  Makame Mbarawa alipokuwa  akifungua  Mkutano wa 19  wa Kamati ya SADC ya usafiri wa Anga uliofanyika jijini Dar es salaam.
“Mkutano huu unalenga kuadhimia kuimarisha usalama wa anga katika nchi za Jumuiya ya SADC, kwa kuwa unahitajika sana kwa wananchi  ili kuongeza shughuli za kiuchumi na kijamii na kuleta maendeleo ya nchi wanachama” alisema Mbarawa
Ameongeza kuwa “ni lazima tuadhimie mambo yatayoleta maendeleo na huduma bora katika usafiri wa anga kwa jumuiya ya SADC ili kujenga uhusiano na malengo yaliyo bora kwa maendeleo ya nchi zetu.”  

Kwa upande wake,  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Bwana Hamza Johari amesema kuwa mkutano huo unalenga kuhakikisha wanafikia na kutekeleza malengo  Jumuiya ya usafiri wa anga wa kimataifa (ICAO) katika kuboresha huduma  za usafiri huo.
“Ni lazima tuyafanyiekazi   maadhimio ya  mkutano huu  ili kuboresha huduma kwa kiwango cha kimataifa pamoja na kuleta unafuu kwa watumiaji wa usafiri wa anga” alisisitiza  Bw. Johari.
Naye,  Mwenyekiti wa SADC Bw. Geoffrey Moshabesha amesema  kuwa  kamati hiyo inajipanga kuunda taasisi ya kiusalama ili kusimamia mifumo yote kwa nchi nzima ili kuweka mazingira mazuri kwa watumiaji wa usafiri wa anga.
Jumuiya ya SADC imeweka  mikakati ya kutekeleza maadhimio hayo katika kuleta usalama wa anga pamoja na kutunza mazingira ili kuboresha huduma kwa watumiaji wa usafiri wa anga kwa nchi wanachama.

No comments