AY NA MWANA FA KULIPWA BILIONI 2.18 NA TIGO BAADA YA KUSHINDA KESIKESI
JANA MAMBO YALIKUWA HIVI
MWAMBAWAHABARIBLOG
Hatimaye kesi iliyounguruma kwa miaka 4 ambayo ilikuwa inawahusisha wanamuziki wawili wakongwe nchini, Ambwene Yessaya ‘AY’ na Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA; dhidi ya kampuni ya Tigo Tanzania imekwisha kwa wasanii hao wawili kushinda kesi hiyo hivyo kutakiwa kulipwa kitita cha Sh Bilion 2.18 kutoka kwa kampuni hiyo ya mawasiliano.
Wasanii hao waliishtaki kampuni ya Tigo kwa kutumia nyimbo zao kama miito (caller tunes) zikiwa na sauti zilizo katika mfumo wa miziki ambayo husikilizwa na mtu anapokuwa akimpigia simu mtu mwingine wakati akimsubiria mlengwa kupokea simu hiyo
Mwana FA baada ya kushinda kesi hiyo amesema kuwa:
“Wakati umefika kwa watu waliokuwa wanatumia hati miliki kwa ajili ya manufaa yao kipindi cha huko nyuma kujua kuwa muda wao umekwisha. Huu ni wakati muafaka wa hatimiliki. Kitu hiki kilikuwa kinafanyika zamani kwasababu tulikuwa hatuna uelewa na kwasababu ya gharama za kuendesha kesi
L EO KUNATETESI KUWA TIGO WAMEKATA RUFAA
L EO KUNATETESI KUWA TIGO WAMEKATA RUFAA
Post a Comment