MOOVN TANZANIA LIMITED YABORESHA HUDUMA ZA USAFIRI.
Na Jacquiline Mrisho
mwambawahabariblog
Kampuni ya Moovn Tanzania Limited
imeboresha huduma za usafiri na kuongeza usalama wa wateja kwa kuanzisha huduma
za usafiri zinazopatikana kwa njia ya mtandao.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es
Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo,Bw.Godwin Ndugulile alipokua
akiwaelekeza waandishi wa habari jinsi ya kujiunga na huduma za usafiri kwa
njia ya mtandao.
“Huduma zetu za usafiri
zinapatikana kwa njia ya simu na tovuti kupitia program za aina tatu ambazo ni
programu inayomuhusu mteja,(Moovn Passenger), programu inayomuhusu dereva
(Moovn Driver) pamoja na Programu inayohusiana na mashirika au makampuni ya
kibiashara”alisema Bw.Ndugulile.
Bw.Ndugulile ameongeza kuwa huduma
hizo zinapatikana bure kwa wateja wote pia kampuni inashirikiana na madereva wa
vyombo vya usafiri wa aina zote zikiwemo taxi, pikipiki, na bajaji ili kutoa
huduma nafuu kwa wateja wao.
Aidha, Bw. Ndugulile amezitaja
baadhi ya faida zinazopatikana kwa kutumia huduma hii kuwa ni; usafiri wa
uhakika kwa kuwa madereva wote wana leseni na wamesajiliwa, usalama, bei
nafuu kulingana na mahitaji na uwezo wa mteja, pamoja na kuongeza ajira na
kipato kwa madereva.
Kampuni ya Moovn Tanzania Limited imeanza
kufanya kazi rasmi Machi 16 Mwaka huu, Ofisi zake zinapatikana maeneo ya
Osterbay Jijini Dar es Salaam pia Kampuni ina mpango wa kufungua matawi mengine
nchi nzima.
Post a Comment