TRL YATANGAZA KUREJEA KWA HUDUMA ZA TREN KUANZIA DAR
mwambawahabariblog
.jpg)
Na John
Luhende
mwambawahabariblog
Uongozi wa
wa kampuni ya Reli Tanzania TRL
umetangaza kurejea tena kwa
huduma zake za kusafirisha abiria
na mizigo kuanzia Dar es
salaam bada ya kusitishwa kwa huduma hizo
January mwaka huu kutokana
na uharibifu wa miundo mbinu ya Reli ulisababishwa na mvua kubwa
iliyo nyesha maeneo ya kilosa
mkoani Morogoro na
Gulwe mkoni Dodoma .
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
kaimu meneja mahusiano wa kampuni hiyo
Mohamedi Mapondela huduma hizo
zina rejea mara baada ya matengenezo kukamilika kwa jihihada kubwa zilizofanywa
baina ya kampuni ya Reli na kampuni hozi ya Reli RAHCO, ambapo matengenezo hayo yali anza
January mosi mwaka huu.
Aidha ameishukuru serikali pamoja na taasisi zake kadhaa kwa jitihada
zilizo fanikisha kurejeshwa
kwa miundombinu ya reli na amewaomba radhi wanachi walipata usumbufu kwa muda wote wa matengenezo kwa
safari zilikuwa ziki ishia Dodoma badala ya Dar es salaam.
Amesema ,ratiba
za safari za treni ya kawaida kutoka Dar es salaam kuelekea Mwanza na kigoma zita kuwa kila siku ya jumanne na ijumaa saa11:00 jioni na
nazile za treni mpya ya Delux,
itakuwa ina ondoka Dar es salaam kila jumapili saa 2:00 asubuhi ,na kutoka Mwanza na Kigoma na treni ya kawaida ina toka
huko kila siku ya Alhamis na Juma pili saa11:00 jion ,tren ya Delux nayo inatoka Mwanza na
Kigoma kila siku ya jumanne saa2:00 asubuhi.
Post a Comment