WAGENI WANAOFANYAKAZI NCHINI BILA KIBALI KUKIONA CHAMOTO
mwambawahabariblogspot.com
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeiagiza Idara ya Uhamiaji nchini kuanza Operesheni maalum ya kuwabaini wageni walioingia na kufanya kazi ambazo sio za kitaalamu zinazoweza kufanywa na Watanzania ilikuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwaondosha.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni baada ya kutembelea Makao Makuu ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar Es Salaam na kuzungumza na makamishna wa idara hiyo.
Akiwa katika ofisi hizo kukagua shughuli zinazoendelea kwenye idara hiyo, Naibu waziri huyo amesema, kumekuwa na ongezeko kubwa la wageni wasikuwa na tija katika nchi ambao wengi wao wamekuja na kuomba vibali vya uwekezaji au kazi za kitaalam badala yake wamekuwa wakifanya kazi na biashara ambazo Watanzania wa kawaida wanaweza kuzifanya.
Naibu Waziri Masauni ameitaka idara hiyo kungalia Upya mchakato wa utoaji wa vibali kwa wageni baada ya vile vya awali kuonekana kuwa na matatizo.
Post a Comment