VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUWAOMBEA WATU WABADILI TABIA MBAYA MFANO WIZI, UVUVI NA UZEMBE
mwambawahabari.blogspot.com
Viongozi wa dini nchini wametakiwa kuwaombea watu wenye nia mbaya
na Taifa la Tanzania ili waweze kuwa raia wema na kuachana na tabia
za kutaka rushwa, uvivu, uzembe na matumizi ya dawa za kulevyia.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mgeni rasmi kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika maombi
maalum ya kuliombea dua Taifa na viongozi, ambaye
ni Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dares Salaam.
“Tabia hizi zimeota mizizi zinahitaji maombi. Tunao
uwezo wa kumwuunga mkono Rais. Kila mtu anao mchango wa kumsaidia Rais
anayoyafanya mfano katika vijiji kutumbua majibu madogo,” alisema
Lukuvi
.
Aliongeza kwamba viongozi hao wanapaswa kuelimisha jamii jinsi ya
kufanya kazi kwa bidii, hivyo wasiache kusisitiza juu ya suala hilo,
likiwemo suala la, amani upendo umoja na mshikamano.
“ Misingi hii ya, upendo, umoja na mshikamano
ilianzishwa na Serikali zilizopita na Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea
kuhimiza juu ya misingi hii, bila ya kujali dini , rangi, kabila, itikadi na
eneo analotoka mtu,” alisisitiza.
Alisema uhuru wa kuabudu utaendelea kuwepo, ila kwa kuzingatia
sheria zilizopo.
Aidha Waziri Lukuvi alisema Serikali itaendelea
kutoa fursa sawa za kiuchumi na kijamii kwa wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya wa Makanisa ya
Pentekoste, ambaye pia ni Askofu wa Huduma ya Tanzania Fellowship Churches
(TFC), Askofu Godfrey Malassy alisema wao kama viongozi wa
dini wako pamoja na Rais John Pombe Magufuli, hivyo hawatamwacha pekee yake katika
mapambano hayo hadi Tanzania itakapokuwa mahali penye neema pa kuishi.
Askofu Malassy aliongeza kwamba ni wajibu wa Watanzania kuomba ili
kuweza kuleta mabadiliko katika Taifa letu.
Alisema madhuni ya maombi hayo ni kumwombea Rais Magufuli
aweze kuendelea kuliongoza Taifa ili liweze kuwa na maendeleo ya
ustawi wa watu wote na liendane na kasi ya kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi tu!.
Askofu huyo alisema mauzo ya kitabu cha ijue siri ya amani na
sadaka zitakazotokana na mkesha huo zitatumika kuelimisha jamii ya ya umuhimu
wa amani, kuendelea kutoa huduma hiyo kwene mikoa ambayo hawajaifikia na kugusa
jamii yenye mahitaji maalum hasa wakina mama na watoto kwa kusaidia kutoa
huduma ya nishati ya umeme.
Post a Comment