TCRA Yavifungia Vituo 27 Vya Radio Na Tv Kwa Kukwepa Kodi
mwambawahabariblog
mwambawahabariblog
MAMLAKA YAMAWASILIANO TANZANIA TCRA imevifungia vituo 21 vya Radio
na 6 vya Television
Vikiwemo vyombo vya SaharaMedia group yaani Star TV, Radio free
Afrika na Kiss
kushindwa kulipa kodi ya lesseni kwa wakati ..
Akitangaza uamuzi huo, mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa TCRA
Innocent Mungy, amesema kuwa mitambo ya vituo hivyo itazimwa ifikapo kesho
saa 6 usiku, na itawashwa baada ya vituo hivyo kulipa madeni yanayowakabili.
Mungy amesema mamlaka hiyo haiwezi kusema ni kiasi gani cha pesa ambacho
vituo hivyo vinadaiwa kwa madai kuwa kanuni na taratibu haziwaruhusu kutaja
kiasi hicho kwa kuwa ni siri kati ya TCRA na mteja.
Aidha Mungy amesema kuwa TCRA imewataka wadau wote wa mawasiliano
nchini kutii sheria bila shuruti na kufuata taratibu, huku akisisitiza kuwa zoezi hilo
la kuwasaka wanaokwepa kodi ni endelevu.
Vituo vingine vilivyofungiwa ni:
- Sibuka FM
- Breez FM
- Country FM
- Ebony FM
- Hot FM
- Impact FM
- Iringa Municipal TV
- Kiss FM
- Kitulo FM
- Kifimbo FM
- Mbeya City Municipal TV
- Radio 5
- Radio Free Afrika (RFA)
- Musa Television Network
- Pride FM radio
- Radio Huruma
- Radio Uhuru
- Star TV
- Rock FM Radio
- Standard FM radio
- Sumbawanga Municipal TV
- Tanga City TV
- Top Radio FM limited
- Ulanga FM
Post a Comment