PICHA ZA MASHINDANO YA BABATI HALF MARATHON
mwambawahabari.blogspot.com
Naibu waziri wa Habari,Utamaduni, sanaa na Michezo Mh Anastazia Wambura akimkabidhi zawadi ya Fedha (shilingi laki tatu) Mshindi wa tatu (kwa wasichana) wa Mbio za Babati half Marathon Rebeka Kwaslema .
Mshindi wa Kwanza wa Mbio za Babati Half Marathon Catherine Langay (kushoto) akiwa na Mume wake Joseph Sulle ambaye pia ni Mshindi wa pili katika mbio hizo kwa upande wa wanaume .
Mshindi wa Kwanza wa Babati half Marathon (kwa upande wa wanaume) Emanuel Giniki akiwa ameshikilia kombe baada ya kukabidhiwa ambapo alikimbia Kilomita 21 kwa sasa 1:07:08
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Anastazia Wambura akimkabidhi Kombe Mshindi wa kwanza wa Mbio za Babati half Marathon Mkoani Manyara kwa Wanawake Bi Catherine Langay ambapo alikimbia mbio hizo za kilomita 21 kwa saa 1:24:30.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh Anastazia Wabura (watatu kutoka kulia) akifuatiwa na Katibu tawala Mkoa wa Manyara Eliakim Maswi (wanne kutoka kulia) wakiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa kisiasa na Wakuu wa Idara mbalimbali.
Mh Anastazia Wambura Naibu Waziri wa Habari utamaduni sanaa na Michezo akimkabidhi Kombe Mshindi wa kwanza wa mbio za Babati Half Marathon Emanuel Giniki.
Naibu waziri wa Habari utamaduni na Michezi Mh Aanastazia Wambura akipuliza kipenga ili kuashiria uzinduzi wa riadha .
Washiriki wa Babati half Marathon wakiwa wanakimbia riadha ya kilomita 21 baada ya Mh Naibu Waziri kuzindua rasmi Mbio hizo leo Mjini Babati Mkoani Manyara Uwanja wa Kwaraa.
Watoto wa kuanzia umri wa miaka 5-15 wakiwa wanajiandaa na kukimbia mbio za kilomita 5 katika mbio za Babati half Marathon.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh anastazia Wambura akitoa Risala yake kwa wananchi wa Wilaya ya Babati na kwa Washiriki wa Mbio za Babati half Marathon ambapo mashindano hayo hufanyika Disema 31 kila mwaka.
Katikati ni Washindi washindi wa kwanza katika Mbio za Babati Half Marathon (kutoka kushoto ni ) Emanuel Giniki akifuatiwa na Catherine Langay wakiwa wameshikilia Vikombe na washiriki wengine wa Mbio hizo wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mh Anastazia Wambura.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mh Anastazia Wambura akimkabidhi zawadi ya Fedha Mshindi wa kwanza wa Mbio za Babati half marathon (kwa wavulana) Emanuel Giniki ambaye alikimbai mbio za kilomita 21 kwa saa 1:07:08. mwambawahabari.blogspot.com
Post a Comment