HAKUNA ATAKAYEBOMOLEWA NYUMBA ALIYEJENGA KATIKA UMBALI UNAORUHUSIWA KISHERIA -KALUA
mwambawahabari
Mbunge wa Jimbo la
Segerea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mh. Bonna Kalua amesema kuwa hakuna
nyumba ya mwananchi itakayobomolewa ambayo imejengwa katika umbali unaohitaji
kisheria wa mita 60 kutoka mtoni.
Mh.Kalua alitoa kauli
hiyo jana jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wananchi wa Karakata
kwenye mkutano wa hadhara.
Aidha alitoa wito kwa
wale ambao wamejenga ndani ya mita 60 na nyumba zao zimewekewa X kujiorodhesha
majina yao kwa wenyeviti wa mitaa ili wamfikishiea Ofisi kwake kwa ajili ya
kulifuatilia jambo hilo kwa ukaribu na hatimaye wapate haki zao.
Mh.Bonna
aliwatahadharisha wananchi kutodanganywa na watu wanaowachangisha fedha kwa
kigezo cha kufungua kesi mahakamani kuwa ni uongo na hawana nia nzuri kwa
wananchi kwa sababu kesi ya bomoa bomoa tayari ilishafunguliwa kwa niaba ya
nchi nzima.
Aliwataka wananchi kuwa
wavumilivu mpaka hapo shauri lilipo mahakamani litakapotolewa tamko .
Post a Comment