Mchungaji aeleza undani ,chanzo na mwisho wa gonjwa la COVID 19.
Mwamba wa habari
Wakati Dunia ikiwa bado imegubikwa na wingu zito la ugonjwa wa COVID 19 unao sababishwa na Virusi vya Corona , hapa nchini kumekuwa na baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii wakibeza na kuhoji ukimya wa watumishi wa Mungu kuhusu ugonjwa huo.
Mchungaji Sindano wa huduma ya MANIM ministry , amezungumza na Mwamba wa Habari na kusema kuwa watumishi wa Mungu hawapaswi kulaumiwa katika hili kwakuwa utaratibu uliowekwa kuhusu wagojwa wa Corona hauruhusu mtu kuonana na mgonjwa bali hutengwa na kuhudumiwa na wahudumu wa afya pekee.
"Hakuna mchungaji aliyepewa nafasi ya kumwombea mgonjwa wa Corona pia huwekumwombea mtu ambaye hanaimani wameaminishwa katika tiba za hospitali, tofauti na utaratibu wa wagonjwa wa magonjwa mengine tumekuwa tukiwaombea na kupona baadhi yenu ni mashahidi tumeombea watu wengi katika mahospitali ikiwemo Amana na watu walipona maana wengine walifungwa na nguvu za giza " Alisema Sindano.
Aidha mchungaji huyo amewaomba wataalam wa afya hapa nchini,kuto yatumainia mataifa ya nchi katika tafiti za dawa bali wafanye tafiti kutokana na mazingira ya nchi .
"Sijambojema kutegemea kilakitu kutoka nje yanchi ilihali kunawataalam waliosomeshwa kwa ghramakubwa na wakabaki kukopi na kupesti" Alisema
Akiwa katika mamlaka ya kichungaji na mtumishi wa Mungu,Mchungaji Evance Sindano amelielezea gonjwa hilo kuwa nigonjwa lililo katika nguvu za giza na kusambazwa na roho chafu ambayo huvaa mtu.
"Imetengenezwa kwa njianne ,kuna roho ya Chura ,ambayo ndiyo unasikia kila sehemu kelele Corona,Corona, pili kuna Roho ya nyoka, hiindiyo inayo tia hofu,tatu roho ya Popo ambayo kazi yake ni kujificha katika mapango ndiyo maana watu wanaambiwa wasalie majumbani wasitoke ,nne roho ya kono kono ndiyo makamasi na makohozi na umeona umbile la hivyo virusi kunamapembe kama ya konokono yalemapembe yake yanaenda yananusa nani mwenyehofu kisha inaingia"Alisema
Amesema katika kutokomeza gonjwa hili amewataka wataalamu kushirikiana na watumishi waMungu katika kupata tiba kwani kunamabo mengine ya kiroho wanaweza kusaidiana pia amemshukuru Rais Magufuli kwa kuliweka taifa mikononi mwa Mungu kwani imesaidia taifa kuwa na umoja wa kuomba kupinga hizo roho ndiyo maana Nchi haijaathrika sana kama zingine .
Hata hivyo amesema Colona itaondoka kwa neno la Mungu kwa kuomba na kusali na kwamba itaondoka kwa muda wa sikusaba ikiwa watu wote watashikamana kwa kuomba.
"Nikiwa kanisani mwaka 2007 niliniwaeleza kanisa juu ya maono nilioneshwa kunaugonjwa umezuka duniani ,lakini waliona kwa kufanya mazoezi ,kunywa maji mengi na kunywa asali , na waliokuwa wanafanyakazi ngumu hawakuugua ila wenye kazi za kukaa waliugua haya yote niliyasema niliita waandishi wa habari lakini hakuna aliyefanyia kazi"Alisema.
Post a Comment