Ads

Kumbilamoto, amwaga msaada wa vifaa vya ujenzi ofisi ya CCM Vingunguti,haijawahi kufanyiwa ukarabati tangu 1972.




Na John Luhende
Mwambawahabari
Diwani wa kata ya Vingungu ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto  leo   ametoa mifuko  15 ya Saruji kwaajili ya ukarabati wa ofisi ya CCM kata ya Vingunguti.

Akizungumza katika eneo la ofisi hiyo Kumbilamoto amesema, amefikia uamuzi huo baada ya kuona ofisi hiyo imechakaa jambo ambalo linasababisha usumbufu kwa viongozi na wanachama hasa wakati mvua.

"pamoja na mifuko hiyo pia nimetoa shilingi million 2 kwaajili ya ujenzi huu, na taka hii ofisi  iwe na kiyoyozi katibu anafanya kazi kuwa sana kwa mazingira ya ofisi hii naona siyo mazuri" Alisema Kumbilamoto.

Kwa upande wake katibu wa CCM kata ya Vingunguti Agatha Gilbert Limbumba amemshukuru Meya Kumbilamoto kwa moyo wake wa kujali na kushiriki kuwa chama hicho kimejipanga vyema kuchukua ushindi kwa mitaa yote.

"Diwani wetu amefanya jambo zuri sana baada ya yeye kujitoa kuanza ukarabati wa ofisi kwa kununua kenchi, Saruji, mchanga, Kokoto mbao na mabati, wilaya nao wameamka wamesema watakarabati upande uliobaki na watanunua mabati" Alisema Agatha

Ofisi ya CCM Vingunguti haijawahi kufanyiwa ukarabati tangu ijengwe mwaka 1972, CCM wilaya  kwa kulifahamu hilo wametoa jumla ya singing million 7 kwaajili ya ukarabati wa ofisi zake katika mitaa ya  miembeni na  mtakuja,

No comments