Barua ya zitto kabwe kwa Katibu Mkuu CPA sakata la Spika Ndugai, Profesa Assad
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA) kumtaka kuingilia kati sakata la Spika wa Bunge, Job Ndugai na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Assad.
Hatua
hiyo imekuja siku chache baada ya spika Ndugai kumtaka Profesa Assad
kwenda mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kinga, Maadili na Madaraka
ya Bunge Januari 21, kwa kitendo cha kuliita Bunge kuwa ni dhaifu wakati
akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa nchini Marekani hivi karibuni,
ambapo amesema akishindwa kufika mwenyewe atafuatwa na pingu.
Katika
barua hiyo, Zitto pia ametuma nakala kwa maspika wa mabunge yote ya
Afrika kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Nchi za
Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC), na Wadhibiti na Wakaguzi Wakuu wa
Hesabu za Serikali wote wa Jumuiya ya Madola, kuwataka kuzungumza na
Spika Ndugai kuachana na kitendo hatari cha kudidimiza misingi ya
uwajibikaji nchini.
“Kwa
kuwa Bunge la Tanzania ni mwanachama wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola
(CPA), naomba uingilie kati kutatua kidiplomasia kwa kuzungumza na Spika
wa Bunge la Tanzania, ukimueleza hatari za uamuzi wake.
“Naamini
kuwa suala hilo linaweza kutatuliwa kwa urahisi na kuboresha uhusiano
kati ya taasisi hizo mbili muhimu yaani Bunge na Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi, ambayo hutegemeana,” imesema sehemu ya barua hiyo ya Zitto.
Post a Comment