Tinga tinga kutafutiwa masoko nchini japani
Na Jesca Mathew
Mwambawahabariblog.
Kampuni ya kijapani
ya Bricoleur Holdings Ltd imesaini mkataba wa miaka mitano na kikundi cha Sanaa
ya uchoraji Tinga Tinga wenye lengo la kuwasaidia wasanii hao kuwatafutia masoko
nchini japani na nchi za jirani .
Akizungumza
na Waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Tanzania BASATA Godfrey Mngereza
amesema kuwa fursa hiyo ni bora na itasaidia kukuza Sanaa ya uchoraji na
kumfanya msanii kupata kipato na kuweza kuchangia pato la taifa kwa kuwa
watakuwa na umiliki halali wa kazi zao.
Naye
mwenyekiti wa chama hicho cha tinga tinga Zachi Zaburi ameishukuru kampuni hiyo
kwani kupitia mkataba huo utaweza kuinua maisha yao kwa kujitangaza kwenye nchi
mbalimbali kupitia uchoraji.
Post a Comment