MHE.BUSSUNGU KUCHUKUA FOMU YA URAIS AGOSTI 10
DAR ES SALAAM
MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha African Democratic Party (ADA TADEA),Georges Bussungu anatarajiwa kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) siku ya jumapili tarehe 10 Agosti,2025.
Tukio hilo muhimu litafanyika Jijini Dodoma katika Ofisi za Tume zilizopo mtaa wa Ndejengwa.
Bussungu ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ADE -TADEA atasindikizwa na viongozi wa chama kutoka ngazi mbalimbali,kitaifa,mikoa na wilaya ikiwa ni ishara ya uhuru , umoja, haki,amani na mshikamano ndani ya chama chenye dhamira ya kuwaletea watanzania maendeleo.
Safari ya kwenda kuchukua fomu itaanzia Makao Makuu ya Chama Ilala Jijini Dar es Salaam kuelekea Dodoma
Aidha,Bussungu ataambatana na Juma Ally Khatibu mgombea Urais Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Chama cha ADA- TADEA kinatumia fursa hii ya kuleta mageuzi kwa kujenga Tanzania mpya yenye utajiri,haki na amani.
Chama Cha ADA-TADEA kina Ilani iliyojikita katika Kauli Mbiu iliyoko kwenye Nembo ya Taifa ambayo ni Uhuru na
Umoja. Hivyo Ilani imezingatia Uhuru, Umoja, Haki, Amani na Mshikamano wa
Watanzania katika kujiletea Maendeleo yao ya kiuchumi, kwa upande mmoja.
Kwa upande mwingine kupambana na vizingiti vikubwa vitatu vya ufanisi na tija ya maendeleo ya nchi
ambavyo ni Upendeleo, Rushwa na Ufisadi (URU).
Mapambano dhidi ya URU yataondoa mtazamo hasi unaotokana na Ubinafsi uliokithiri. Hii inathihirika kwenye Matendo yetu, Misemo yetu na hata Maandishi yetu kuwa Serikali inayochaguliwa ni mali ya Chama na
siyo ya Wananchi. Utofauti wetu na Vyama vyote vya Siasa nchini ni “Umoja na Utanzania”ambayo ni Kauli Mbiu yetu kwamba “Usawa kwa Jamii” yaani Binadamu wote ni Sawa na kila mtu
anastahili kula keki ya nchi kwa heshima akiwa huru kwenye nchi yake HURU.
Serikali ni ya Watu inawajibika kwa Watu, kwa kuwa imechaguliwa na Watu yaani Watanzania wote. Kwa mantiki hiyo, hapo ndipo Dira yetu ya Ilani ya Uchaguzi wa Mwaka 2025 iliposimamia.
Tanzania Mpya ya kisasa inayojitegemea yenye Utajiri, Haki, Weledi, Amani, Upendo na Uchumi bora kwa Wananchi wake kuliko nchi zote katika Afrika.
Dhamira ya Chama cha ADA -TADEA;ni Kuwawezesha wananchi kwa haki na usawa kujitajirisha kutokana na fursa na raslimali zilizopo nchini kwa njia halali kwenye sekta zote za kiuchumi ili nchi iwe ya Uchumi wa juu na Maisha Bora kwa kila Mtanzania.
Kwa mantiki hiyo kauli mbiu ya ADA-TADEA kwa uchaguzi wa mwaka 2025 ni Uhuru na uwajibikaji,Ni utekelezaji wa Kauli Mbiu hiyo ndio itasababisha kufanikisha ujenzi wa Tanzania mpya yenye utajiri,Haki na Amani",
Post a Comment