TEMBELEA BANDA LA DORKIN KUPATA ELIMU YA VYAKULA VYA ASILI
Na Mwandishi wetu Mwamba wa habari
DAR ES SALAAM
MKURUGENZI wa Dorkin Ofganic Farming Co.LTD,Prof.Dorcas E.Kibona anawawakaribisha watanzania wote kutembelea Banda lao katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (SABASABA) yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius K.Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Prof.Kibona amewakaribisha wananchi leo Julai 5,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kwamba watakao tembele hapo watapata elimu na faida zakutumia vyakula vya asili ambavyo vinaleta afya bora.
Aidha ,amesema kwamba wamejipanga ipasavyo kutoa elimu ya vyakula vya asili hususani ndizi tirisa pamoja na mbegu bora za asili.
"Tumekuja na uji wa maajabu onya upone, ambao umefanya vizuri na wengi wamekunywa na wanaokunywa wameenda nyumbani na wamewaita wengine",kituo kinafanya vitu ambavyo ni halisi,ukweli na vyenye uhakika ndani yake",amesema Kibona
Pia, ameeleza kwamba kituo kimejipanga sana kwenye kilimo hai kwa sababu afya imeanzia sana kwenye ardhi,kama ardhi imekosa na ukalima kile ambacho kinatakiwa kuliwa hivyo mlaji anaweza kupata changomoto ya magonjwa ya sukari,presha , saratani ,nguvu za kike na kiume mlaji anatakiwa kufahamu anakula nini,anakunywa Nini,usipoangalia unachokula ama unachokunywa mwisho wa siku utakuja kudumbukia kwenye wimbi la magonjwa yasio na maambukizi.
Hata hivyo,wanatoa elimu Bure kwenye kituo Cha ushauri Salasala kwa ajili ya afya zetu wapo kwenye kituo cha shamba darasa eneo la Salasala,unapata elimu Bure,mbegu Bure pamoja na kupata mafunzo ya kilimo hai.
Sanjari na hayo pia wanaprogamu maalum kwa ajali ya vijana waliohitimu kama wanaelimu ya masoko watapata elimu ya masoko jinsi kufanya biashara.
Aliendelea kwa kusema kwamba kituo kimejipanga ili waweze kuwafikia watanzania takribani milioni moja na mpaka sasa katika maonesho yanayoendelea wamefanikiwa kutoa elimu kwa wananchi takribani laki moja.
Post a Comment