Ads

WANANCHI DAR WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUPATA MSAADA WA KISHERIA WA MAMA SAMIA .

 


*WALIO HUDUMIWA  KATIKA BANDA  LA MWANASHERIA MKUU WA SERIKLALI WAPONGEZA UBORA WA HUDUMA*.

Wanasheria kutoka ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali wakiendelea kutoa huduma ya kisheria kwa wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Maturubai  Mbagala Temeke Jijini Dar es salaam


Na John Luhende

Wakili wa Serikali mkuu Grace Thadei Komba , ametoawito kwa wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kufika kupata msaada wa kisheria katika viwanja vya Maturubai Mbagala Kizuiani Wilayani Temeke kabla ya muda uliowekwa kufikia mwisho.


Komba ametoa wito huo leo wakati akizungumza na Waandishi wa habari  kuhusu maendeleo ya na mwitikio wa wananchi katika kampeni ya msada wa kisheria wa Mama Samia (Mama Samia legal Aid campaign) iliyozinduliwa na Waziri Mkuu  wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe, Kasim Majaliwa tarehe 16 June 2025 .

 

,,Mwitikio ni mzuri ila naendelea kuwahimiza walewote wenye matatizo ya kisheria ambao bado hawajafika hapa wafike mapema maana siku zimebakia chahe, waje wahudumiwe natimu kubwa ya wanasheria na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikotayari kuwahudumia''Amesema Komba.


Amesema kampeni hii ya msada wa kisheria wa Mama Samia, inayosimamiwa na Wizara ya katiba na Sheria itaendelea hadi Juni 27,na ofisi ya Mwanansheria Mkuu wa Seriklai iko hapa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwahudumia wananchi.


Baadhi ya wananchi waliofika leo kupata huduma ya kisheria  katika banda la ofisi ya Mwanansheria Mkuu wa Serikali wameipongeza Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta kampeni ya kisheria huku wakiwapongeza wanansheria ambao wamejitoa kuwahudumia na kuwapa muda wa kuwasikilza bila upendeleo.


''Kwanza kabisa namshukuru sana Rais Samia mimi ni Mwananchi wa kawaidatu, siwezi kumudu gharama za kumlipa wakili lakini nimefika hapa nimepokelewa vizuri na nimepewa muda wa kusikilizwa  naondoka moyo wangu ukiwa na matumaini kwamba jambo langu linashugulikiwa kisheria na haki itatendeka'' Amesema  Adolf Shirima  mmoja wa wananchi walipatiwa huma ya kisheria.






No comments