URUSI YASITISHA MAPIGANO KUFUNGUA NJIA ZA KIUTU.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kuwa jeshi la nchi hiyo litasitisha mapigano na kufungua njia za kiutu kwenye miji kadhaa ya Ukraine ili kuruhusu raia kuondolewa kwenye maeneo hayo.
Wizara hiyo imesema njia za kiutu zitafunguliwa kwenye miji ya Kiev, Kharkiv, Mariupol na Sumy. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wale wanaotaka kuondoka Kiev wataweza kusafirishwa pia kwa kutumia ndege hadi Urusi.
Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na ombi lililotolewa na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.
Ukraine imesema msimamo wa Urusi kuhusu njia za kiutu ni kinyume na maadili kabisa.
Wakati huo huo, wapatanishi wa Ukraine na Urusi wanatarajiwa kukutana leo kwa mazungumzo.
Hata hivyo, muda kamili na eneo yatakapofanyika mazungumzo hayo bado haujatangazwa.
Mara ya mwisho wajumbe wa nchi hizo mbili walikutana nchini Belarus katika duru mbili za mazungumzo ya amani.
Kwa msaada wa DW
Post a Comment