MAPYA KUHUSU TAASISI YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE/ MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA BABA WA TAIFA.
Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere inatarajia kufanya makongamano ya kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kumbumkumbu ya miaka miamoja tangu Kuzaliwa kwake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini
Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Paul Kimiti, amesema kuwa ifikapo
Aprili 13 Baba wa Taifa atakua anatimiza miaka100 tangu kuzaliwa, hivyo
makongamano hayo yatafanyika kikanda yakienda sambamba na kufanya shughuli za
kumuenzi baba wa Taifa pamoja na Upandaji wa miti.
Amesema kuwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere enzi ya uhai wake alisimamia falsafa ya kulinda amani,
kuondoa ubaguzi, na kuwafanya watanzania waweze kuishi kwa upendo na kujitegemea.
Amesema kuwa falsafa hizo zinapaswa kuenziwa
kupitia Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu nyerere ili kuwafanya vijana na jamii
kwa ujumla kuzifahamu.
Mwekiti Kimiti ameongeza kuwa wanapaswa
kuendelea kuzijua kazi alizozifanya baba wa Taifa katika kulikomboa Taifa na
kwamba kuenzi juhudi hizo kutalifanya Taifa kuendelea kulinda misingi ya amani,
mshikamano na upendo na kuondoa ubaguzi miongoni mwa jamii ya kitanzania.
“Mwalimu Nyerere angekua hai April 13
anatimiza miaka mia moja tangu Kuzaliwa kwake, tumeamua kufanya kumbukumbu ya
Kuzaliwa kwake kwa kufanya makongamano ambayo yatafanyika kikanda na tutafanya
shughuli Mbalimbali za kumuenzi kikanda” amesema Kimiti.
Ameeleza kuwa watanzia kanda ya Ziwa pale
Butiama alipozaliwa, kanda ya kati, kanda ya kaskazini, kanda ya kati Dodoma,
Dar es salaam, Kanda ya kusini pamoja na kanda ya Magharibi.
Amefafanua kuwa kila kanda watafanyika
shughuli za upandaji miti pamoja na makongamano yatakayozungumzia falsafa za
mwalimu kulingana na historia ya mikoa iliyopo kwenye kanda hizi na jinsi
ilivyohusika katika kuendeleza kudumisha amani, upendo na mshikamano.
Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Simon Lubugu,
amesema kuwa viongozi waliopo kwa sasa ni wale waliozaliwa miaka ya hivi
karibuni, hivyo hawajui misingi ya baba wa Taifa ilivyokua.
Amesema kuwa kupitia Taasisi hiyo watapata
fulsa ya kujua misingi ya Baba wa Taifa aliyowajengea watanzania email ya uhai
wake.
“Viongozi wengi wa sasa wamezaliwa miaka ya
themanini, hivyo wamekua sio wazalendo kwa Taifa kwa sababu hawajui misingi
iliyoachwa na muasisi wa Taifa hili” amesema Bw. Lubugu.
Amesema kuwa kuanzishwa kwa Taasisi hii
itasaidia sana vijana waliozaliwa kipindi hiki na kijacho kufahamu misingi hiyo
iliyoachwa na Baba wa Taifa.
Mjumbe wa Taasisi hiyo Ummy Wenceslaus, amewataka
vijana kuona umuhimu wa kujiunga na Taasisi kutokana na mchango wa baba wa
Taifa hili na mataifa mengine hasa katika kujenga misingi ya amani, mshikamano
na upendo miongoni mwa watanzania.
Amewataka wasanii kutumia sanaa zao kupaza
sauti juu ya kumuaenzi baba wa Taifa katika jamii ili kuendeleza mazuri ambayo
ameacha Kama alama ya upendo kwa Taifa, huku akiwaasa pia viongozi kuyaishi kwa
vitendo yale yote aliyoanzisha baba wa Taifa.
“Ni vyema viongozi wa sasa waishi falsafa ya
baba wa Taifa kwa vitendo kwani falsafa zake zimesaidia kuleta ukombozi kwa
Taifa na mataifa mengine Barani Afrika” amesema
Hata hivyo wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Taasisi hiyo, Balozi Mstaafu Francis Mndolwa, pamoja na Mhamasishaji Mtiti Mbassa Jirabi ambao kwa nyakati tofauti wameelezea umuhimu wa kumuenzi baba wa Taifa hayati Julius Kambarage Nyerere.
Post a Comment