SIMBA YACHEZEA KICHAPO MBELE YA CHAMA
Klab ya Simba Sc ya Jijini Dar es salaam, imejikuta ikichezea kichapo cha aibu katika mchezo wake wa kwanza kwenye ligi baada ya kumalizika kwa michuano ya Mapinduzi baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mbeya City kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Sokoine Jijini Mbeya.
Mbeya City walifanikiwa kupata bao lao la pekee kupitia kwa mshambuliaji wao Paul Nonga ambaye alipachika bao hilo dakika 20 ya mchezo katika kipindi cha kwanza mara baada ya kuwazidi nguvu mabeki wa Simba Sc ambao inasemekana walizoea kula urojo Zanzibar.
Mbeya City ikiwa imara ilicheza pungufu toka kipindi cha kwanza mara baada ya nahodha wao kupata kadi mbili za njano na kuwafanya Mbeya City kucheza jihadi.
Licha ya kucheza pungufu Mbeya City ilionekana kuwa vizuri kuzuia ambapo kipa wao Dida Munishi alionekana shujaa kwa kuokoa michomo lukuki kutoka kwa washambuliaji wa Simba Sc.
Simba Sc ilipata penati iliyozua utata dakika 49 ya mchezo, ambayo ilienda kupigwa na Chris Mugalu ambaye alifanikiwa kugonga mwamba na kushindwa kuingia kambani.
Baada ya mchezo huo mashabiki wa timu ya simba walisikika wakitaka mchezaji wao Pape sakho aingie kucheza ambaye aliingia japo naye hakuonesha maajabu yoyote , baada ya kuona hilo walitaka tena Chama acheze japo hakuwa hata katika orodha ya wachezaji wa leo.
Hapo jana mahasimu wao Yanga Africans walipata ushindi mnono wa magoli 2-0 dhi ya timu ya Costal Union ya Tanga katika uwanja wa Mkwakwani.
Post a Comment