Ads

MKUU WA MKOA RUVUMA ASISITIZA UTOAJI WA RISITI ZA EFD NA ELIMU YA KODI KWA WAFANYABIASHARA

Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Msafiri Mbibo akiongea na wafanyabiashara wa Mkoa wa Ruvuma wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani hapo yenye lengo la kupata taarifa ya tathmini kuhusu maadili na utoaji huduma ikiwemo kuzungumza na walipakodi.

Wafanyabiashara wa Mkoa wa Ruvuma wakifuatilia hotuba ya Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Msafiri Mbibo wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani hapo yenye lengo la kupata taarifa ya tathmini kuhusu maadili na utoaji huduma ikiwemo kuzungumza na walipakodi.

Mwambawa habari 

MKUU wa Mkoa wa RUVUMA, Mhe. Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amewataka wafanyabiashara mkoani Ruvuma kuhakikisha kwamba wanatoa risiti halali za EFD kwa wateja wanaowauzia bidhaa ama kuwapa huduma mbalimbali.

Kauli hiyo ameitoa jana ofisini kwake wakati alipotembelewa na Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mbaye alikuwepo mkoani hapo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kupata taarifa kuhusu tathmini ya maadili na utoaji huduma kwa walipakodi.

Mhe. Ibuge amesema kuwa, wauzaji wengi wanawazungusha wanunuaji wa bidhaa pindi wanapodai risiti hali ambayo inapelekea ukosefu wa mapato ambapo ameitaka pia TRA kuhakikisha kwamba inatoa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu suala la umuhimu wa utoaji wa risiti na kudai risiti halali.

“Kudai risiti ni jukumu la mnunuzi na kama ilivyo katika kutoa risiti ni jukumu la muuzaji, sasa kuna katabia ya kusingizia mashine imeharibika kumbe hawataki kutoa risiti, kwahiyo katika eneo la utoaji wa risiti za EFD tunayo kazi ya kufanya”, alisema Ibuge.

Kwa upande wake Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Msafiri Mbibo amesema kwamba lengo la mkutano ni kusikiliza kero za wafanyabiashara pamoja na kujenga mahusiano mazuri na kushauriana kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kodi ili makusanyo ya mapato Yazidi kuongezeka.

“Sisi TRA mnapotupatia kero zenu tunazipokea kama hoja ili tuweze kuzifanyia kazi na tunalo jukumu la kuhakikisha kwamba tunajenga uchumi katika kaya moja moja na jamii kwa ujumla”, alisema Mbibo.

Baadhi ya Wafanyabiashara mkoani hapo wameeleza baadhi ya changamoto zao hususani katika makadirio, marejesho ya gharama za ununuzi wa mashine za EFD pamoja na masuala mengine yanayohusua VAT na hivyo wameiomba TRA kuwasaidia kuwatatulia changamoto hizo ili waweze kulipa kodi zao stahiki.

Naibu Kamishna Mkuu wa TRA yupo ziarani katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma pamoja na Njombe kwa lengo la kutembelea ofisi za TRA na kupokea taarifa ya tathmini ya maadili katika ulipaji wa kodi na utoaji huduma kwa ujumla.

No comments