MFUMO WA TIKETI RAFIKI ZA MABASI YA MIKOANI WAZINDULIWA RASMI.
Mkurugenzi wa kampuni ya Global Light and Company Limited Bw Raymond Magambo akielezea namna mfumo mpya wa wa Tiketi rafikiutakavyo fanya kazi
Mkurugenzi wa kampuni ya Global Light and Company Limited Bw Raymond Magambo katikakati akishiriki tukio la kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Tiketi Rafiki wengine ni viongozi kutoka vyama mbalimbali vya wamiliki wa Mabasi ,Makalani , Mawakala na kutoka kampuni ya Global Light and Company Limited.
Na John Luhende
Wamiliki wa Mabasi na wadau wa usafiri nchini wametakiwa kuupokea mfumo mpya wa wa Tiketi rafiki na kuwasisitiza watanzania wengine ili kuondoa changamoto zilizopo hivi sasa katika sekta ya usafirishaji abiria.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya Global Light and Company Limited Bw Raymond Magambo wakati wa uzinduzi wa mfumo wa Tiketi Rafiki uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Akiuzungumzia mfumo huo mkurugenzi huyo amesema nimfumo unaotambua thamani ya Wakala na Kalani katika huduma ya ukataji Tiketi na umejizatiti kufanya kazi kwa ukaribu na mawakala ama kushirikiana nao.
''Mfumo huu umekuwa ukipigwa vita na mawakala wakidhani kwamaba utaenda kuchukua kazi zao, lakini hii ni tofauti kabisa tutaenda kufanya kazi nao na kuona namna gani tunakwenda kuboresha maisha yao na fursa za o za kiuchumi''Alisema
Amesema Tiketi Rafiki itaenda kuboresha kiwango cha utoaji huduma katika sekta ya utoaji huduma wa Abiria kuwezesha kuwa na njia rahisi , salama na yenye uhakika utakao wawezesha watoa huduma kufanya shughuli zao kirahisi .
''Tunafahamu kabisa changamoto zilizopo kwasasa unapo kwenda kwenye vituo vya Mabasi kwenda kubook Tiketi inakuwa ni mchakato watu wanavutwa huku na kule ni vurugu ''Alisema .
Kupitia mfumo huu mtu anaweza kupata huduma ya Tiketi yake akiwa nyumbani wakati wowote iwe usiku au mchana pia Wakala anaweza kupata stahiki yake bila shida yoyote na hata wenye mabasi wanaweza kupata sehemu yao pasipo kupoteza mapato kama ilivyo hivi sasa.
Mfumo huu hasa upo katika sehemu kuu tatu ,kuna Website itakayo muwezesha mtu kukata Tiketi ,kna APP ya simu itakayo wezesha pia kukata Tiketi na jia nyingine ni kuwaona mawakata watakuwa na shine maalumu (POS) njia hii wanaweza kutumia ambao hawana simu.
Na John Luhemde
Pamoja na hayo amesema kupitia mfumo huu mawakala wataweza kuunganishwa na Mabank na kuweza kupata mikopo na hii itawasaidia kukuza uchumi pia wataunganishwa na watu wa Bima wanaweza kupata Insurance na watu wa mifuko ya kijamii (Pension Funds) na sasa mawakala hawa ambao walikuwa wananonekana wapiga debe watakuwa katika mfuko rasmi.
''Kupitia Tiketi Rafiki Serikali itapata mapato yake kila zinapo katwa tiketi kwa mfumo huu ''Alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wamiliki wa Mbasi Mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Ndamba Trans , Musa Ngo'mbo amesema wameupokea mfumo huu na kuitaka kampuni ya Global Light and Company Limited kuendelea kutoa elimu zaidi ili wanchi waweze wauelewe vizuri zaidi .
Naye mwenyekiti wa Chama cha Mwakala na Makalani wa Mabasi mkoa wa Dar es salaam Bw Hamisi Juma Idd amesema , wako tayari kuisapoti Serikali kupitia mfumo huu.
Post a Comment