TISHIO UKATILI WA KIJINSI WILAYA YA KIBITI / KANISA LA KKKT - DMP YATOA SOMO KWA WANANCHI MKOA WA PWANI
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bungu A, Mjawa na Jaribu Mpakani wakifanya wakiimba kwaya yenye maudhui ya kupinga Ukatili wa Kijinsia katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili yaliofanyika Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani
NA NOEL RUKANUGA, PWANI.
Viongozi mbalimbali
wakiwemo Wabunge na Madiwani wametakiwa kubuni mfumo imara wa sera na sheria kwa
ajili ya kuzuia ndao za utotoni, kuwalinda watoto walioolewa pamoja na kutoa
mwongozo katika kutekelezaji ili kuhakikisha uwajibikaji kulingana na
ilivyodhamiriwa katika ngazi ya taifa na kimataifa.
Akizungumza katika Maadhamisho
ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia, yaliofanyika Wilaya ya Kibiti Mkoani
Pwani, Afisa Miradi Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania -Dayosisi ya Mashariki na Pwani (KKKT - DMP), Msimamizi
wa mradi wa Kupinga ukatili wa kijinsia
kupitia jukwaa la dini mbalimbali unaotekelezwa kwa ubia na Shirika la Msaada
la Norwey (Norwegian Church Aid -NCA). Bi. Agatha Lema.
Amesema kuwa wabunge na madiwani
wapo katika nafasi ya kipekee ya kuendeleza na kutekeleza mfumo katika nchi pamoja
na kuhakikisha sauti za wananchi zinasikika ikiwa ni pamoja na watoto wa kike ili
waweze kuhamasisha utashi na dhamira ya kisiasa ya kukomesha ndoa za utotoni.
“Sababu za msingi ndoa za utotoni ni kutokuwepo usawa wa kijinsia na thamani ya chini wanayopewa wasichana, hali hii inaongezeka kutokana na umaskini, kukosekana usalama wa mtoto wa kike na kuwepo migogoro ndani ya ndoa” amesema Bi. Lema.
Bi. Lema ameeleza kuwa
ukatili wa kijinsia unachochewa na sehemu kubwa ya kanuni zisizo sawa za kijinsia
na kichangia ni ukiukwaji wa haki za binadamu.
Amesema kuwa ukatili
umeathiri watu katika sehemu tofauti katika maisha yao ikiwemo kimwili, ki-ngono,
kihisia, huku sababu nyengine zikieelezwa ni hali ngumu ya maisha, tama,
wanawake kuwategemea wanaume kupita kiasia pamoja na mila na desturi.
Amefafanua kuwa katika
kupambana na kukatili wa kijinsia kanisa la KKKT kwa kushirikiana na wadau
maendeleo Norwegian Church (NCA) wamefanikiwa kutoa elimu katika shule za
msingi za Bungu A, Mjawa na Mpakani.
Bi. Lema amesema pia
wametoa elimu kwenye kamati tano za kupinga ukatili kwa wanawake na watoto
(MTAKUWWA), Mabaraza ya Usuluhishi katika Kata ya Bungu, Mjawa, Kibiti zilizopo
Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.
Amesema kuwa wameendelea kukihudumia
kituo cha kutoa msaada wa kisheria cha (Paralegal) Kibiti ambapo kesi nyingi wanazopokea
ni migogoro ya ndoa, matunzo ya watoto, talaka, ardhi pamoja na kesi za madai.
Amesema kuwa KKKT na NCA
wameendelea kufanya kazi kwa karibu katika Wilaya ya Kibiti na dawani la
kijinsia la Polisi, Mahakama na wanasheria wa Wilaya pamoja na madaktari katika kutoa elimu ya kijamii na
makuzi kwa vijana.
“Ili kuendelea kufuchua
uovu na ukatili wa kijinsia tumefanya kazi kwa karibu na vyombo mbalimbali vya vya habari ili
kuendeleza mijadala kuhusu ukatili wa kijinsia” amesema Bi. Lema.
Amesema kuwa wamegundua
kuna ongezeko la mimba za utotoni, ulawiti kwa wanandoa, wanafunzi wa kiume na
wa kike, utelekezaji wa watoto unapelekea kwa kukosa huduma na kujiajiri katika
umri mdogo.
KKKT - DMP, na NCA wanatekeleza
miradi mbalimbali ikiwemo Utawala Bora (PETS), Uwezeshaji wananchi kiuchumi
kupitia IT Vicoba, utoaji wa msaada wa kisheria kupitia vituo vilivyopo katika
Wilaya za Kibiti, Rufiji, na Mafia na kamati za,mahusiano ya dini mbalimbali za
Wilaya, kamati za wanawake na vijana.
Amebainisha kuwa kwa sasa
wanatekeleza mradi wa miaka minne wa kupiga vita Ukatili wa Kijinsia kuanzia
2020 hadi 2024.
Akizungumza katika
Maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kapten Jenerali Ahemed Abas Ahemed,
ametoa agizo kwa Wananchi kuwa na udhubutu wa kutoa taarifa kwa Madawati ya
Kijinsia pale wanapofanyiwa vitendo hivyo.
Amesema kuwa elimu juu ya
ukatili wa kijinsia inayotolewa na wadau ni lazima ifanyiewe kazi, kwa kuwa
kufanyiwa ukatili bila kutoa taarifa haitasaidia kukomesha vitendo hivyo.
Amewataka wanaohusika na
kupokea taarifa hizo kutunza siri za watu akidai kuwa kusambaza taarifa hizo kunaweza
kuchangia watu kuogopa kutoa taarifa hizo kwa kuona wanadharirishwa.
Amewashukuru wadau wote
wanaofanya kazi ya kupinga ukatili wa kijinsia Wilayani humo ikiwemo Dayosisi
ya Mashariki na Pwani huku akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano.
Afisa Ustawi wa Jamii
Wilaya ya Kibiti Jacob Kashinde, amewaomba wazazi, walezi na jamii kwa ujumla
kushiriki kikamilifu kukomesha vitendo vya ubakaji na mimba za utotoni ambazo
zinaongezeka katika maeneo hayo.
Mkuu wa Dawati la Jinsia
na Watoto Wilaya ya Kibiti Jovitha Mulima, amesema kuwa ili kukabiliana na
vitendo hivyo lazima lianze ngazi ya familia, taarifa zitolewe mapema katika madawati
ili zifanyiwe kazi, wananchi wawe tayari kutoa ushahidi wanapohitajika.
Ameshauri suala la ngoma
katika maeneo hilo lazima litazamwe upya licha ya kudumisha tamaduni, lakini
kuna vichocheo vingi vinavyopelekea ubakaji na ulawiti kwa watoto kupitia ngoma
hizo.
Maadhimisho ya siku 16 za
kupinga ukatili wa kijinsia yamefanyika kimkoa wa Polisi Rufiji katika Wilaya
ya Kibiti kata ya Bungu Mkoa wa Pwani, ambapo yameongozwa na kauli mbiu inayosema
Mtoto wa Kike sio Bibi Arusi.
Post a Comment