Waziri Mwambe aitaka mikoa kutekeleza Miongozo ya Uwekezaji
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Geoffrey Mwambe, (katikati) akiangalia uzalishaji wa bidhaa katika Kiwanda cha uchakataji Mafuta ya kula cha Jielong, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, na kulia ni Meneja wa kiwanda hicho Shang-Jie.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Geoffrey Mwambe (kulia) akisikiliza maelezo yamtambo wa uzalishaji bidhaa kwenye kiwanda cha Jambo Food Products Ltd, kutoka kwa mwekezaji wa kiwanda hicho Salum Khamis. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema na Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko,
Waziri wa NChi Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji ameitaka mikoa ambayo tayari imeandaa miongozo ya fursa ya uwekezaji itekeleza kikamilifu miongozo hiyo kwa kuandaa mikakati ya utekelezaji wa miongozo hiyo ikiwemo kutenga maeneo ya uwekezaji na kuyaendeleza kwa kadri inavyofaa kwa ajili ya uwekezaji.
Waziri Mwambe amebainisha kuwa utekelezaji wa miongozo hiyo utahamasisha na kuvutia uwekezaji katika mikoa hiyo kwa kutangaza fursa za uwekezaji hali itakayoisaidia mikoa hiyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kujitangaza kimataifa kupitia fursa zilizopo nchini hali itakayosaidia uwekezaji kuwa na tija kwa Taifa
Akiongea wakati wa kuhitimisha ziara yake mkoani Shinyanga Mhe. Mwambe amefafanua kuwa utekelezaji wa miongozo hiyo kutaongeza kasi ya wawezekezaji kuja Tanzania na kuwekeza katika maeneo ya vipaumbele vya mikoa husika.
Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa ambayo imeandaa Mwongozo wa uwekezaji katika sekta ya madini, mazao yatokanayo na mifugo, kilimo na usindikaji wa mazao.
“Shinyanga ni mkoa ambao kijiografia na kibiashara, upo katika sehemu nzuri na kuna kila sababu ya kuutekeleza mwongozo wenye kuainisha fursa za uwekezaji zilizopo katika mkoa huu na kutenga maeneo ya uwekezaji pamoja na kuyaendeleza ili kuwavutia wawekezaji” amesema Mwambe.
Katika hatua nyingine Mhe. Mwambe ametembelea wawekezaji katika kiwanda cha Jambo Foods Limited na Jielong, ambapo ametoa wito kwa wakazi wa mkoani shinyanga kuchangamkia fursa za uwekezaji wa viwanda hivyo kwa kulima mazao ambayo yanatumika kama malighafi ya viwanda hivyo.
Mhe. Mwambe amefafanua kuwa serikali imehamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza nchini na kutumia malighafi za hapa nchini, lengo ni kuhakikisha wananchi wanainuka kiuchumi.
Post a Comment