WAUMINI DINI YA KIISLAMU WATAKIWA KUMRUDIA MUNGU KUEPUKA MAJANGA.
Na
Mwandishi wetu.
WAUMINI
wa
kiislamu na watanzania kwa ujumla wametakiwa kumrudia Mungu ili awaepushe na
majanga yanayolisibu Taifa na Dunia kwa ujumla.
Akizungumza katika maadhimisho
ya kuzaliwa kwa Mtume (SWA),Imamu Mkuu wa msikiti wa Tambaza Shehe Athuman
Mohamed amesema Tanzania na Dunia kwa ujumla inapitia kipindi kigumu sababu ni
kumuacha Mungu.
“Tunapoadhimisha mazazi ya
Mtume ni lazima tujirudi nakujitathimini wapi tumekosea tutubu, tufanye dua
atuondolee balaa ambalo linalikumbaTaifa, ikiwemo ukame, Covid 19 na mengineyo,
tukitubu na kuomba yote yanakwisha”amesema
Shehe Mohamed amesema siku
hiyo huadhimishwa zaidi kwakupokkea mawaidha ya mtume, kusifu, kuombea amani ya
nchi na dunia kwani Mtume kila alipokwenda alihubiri amani.
Shehe Mohamed aliwataka
vijana kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani ikwemo wizi, matumizi
mabaya ya mtandao, kutumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa wasiolitakia mema
Taifa na badala yake wamuunge Rais Samia Suluhu Hassan kwakuchapa kazi ili
kujiletea maendeleo.
“Kama kuna kundi lolote
duniani hutegemewa zaidi katika kuliletea Taifa maendeleo vijana ni injini
inayotegemewa ,lakini wakitumiwa vibaya basi uasi,uhasama na machafuko ni
rahisi kutokea”alisema, vijana wajikite zaidi kwenye uzalishaji mali nakumrudia
Mungu”alisema
Hata hivyo Shehe Mohamed
aliihakikishia serikali kuwa Msikiti wa Tambaza na BAKWATA kwa ujumla wanafanya
kazi bega kwa bega kuhakikisha amani inapatikana katika Taifa hili kwa minajili
yakukemea uovu ikibidi hata kuwafichuwa waovu.
“Hatupo tayari kuona amani
ya nchi hii inavurugwa ,kama viongozi wa dini tutapaza sauti zetu katika
kukemea uovu na uhalifu kupitia majukwaa yetu ya ibada, lakini pia niwakumbushe
wananchi kushiriki sensa ya mwakani kwani pasipo kuhesabiwa tutakwamisha
mipango na mendeleo yetu wenyewe” amesema
Kwaupande wake msaidizi wa
Maalimu Badrusalum Omary amesema maadhimisho hayo ni muhimu kwani hakuna
wakuenziwa kama Mtume na wanaadhimisha kwa sababu ya mazuri waliyotendewa na
Mtume.
“Katika maadhimisho haya
kikubwa ni kukumbushana kuwa wanyenyekevu , waadirifu na kuombeana dua zenye
heri na kutoa misamaha nakupokea misamaha kwani Mtume alikuwa mwingi wa rehema
na mwenye kusamehe zaidi sisi ninani hadi tusisamehe”amesema
Hata hivyo Maalim Omary
anawataka wazazi kuwa karibu na Watoto wao ili kujua nini wanafanya wawapo
mtaani na nini wanfanyiwa na pia kushirikisha viongozi wa dini pindi
zinapotokea changamoto za kinidhamu ili viongozi wadini wawasaidie wazazi
katika malezi bora.
Naye muumini wa msikiti
huo ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) anayesoma
Shahada ya kwanza ya Uhasibu Aljabir Nzali aliwataka vijana wenzake na jamii
kwa ujumla kumrudia Mola kwani ndiyo kila kitu.
“Nimefika hapa nilipo mwaka wa tatu sasa sis jambo rahisi, lakini si kwa uwezo wangu, walimu na wahadhiri au wazazi bali ni kwa uwezo wa Mola hivyo tumrudie yeye ndiye kila kitu katika maisha yetu.
Post a Comment