Ads

RC MAKONDA ATOA MSAADA WA MABATI YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 476 KWAAJILI YA KUEZEKA NYUMBA 1,000 ZA WAJANE WALIOKUMBWA NA ADHA YA MAFURIKO DAR


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* ametoa *msaada wa Mabati yenye Thamani ya shilingi Milioni 476 kwaajili ya Kuezeka Nyumba 1,000 za Wajane* mkoani humo ambao *nyumba zao zimeathiriwa na mafuriko* yanayotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha ambapo amewataka *Wananchi waliojenga mabondeni kuondoka.*

*RC Makonda* amesema hayo wakati wa *Ziara ya Kukagua athari za Mvua*  na kubaini *uwepo wa familia za Wajane* ambao *Nyumba zao zimechukuliwa na Mafuriko* na sasa wanapitia changamoto ya *kuhifadhiwa kwa majirani* baada ya *kukosa makazi ya kuishi* hivyo ameona ni busara kutoa msaada huo kama sehemu ya *pole kwa adha waliyoipata.*

Aidha *RC Makonda* amewapa *siku 10 Wakuu wa Wilaya* kuhakikisha *wanapitia maeneo ya Mito na Mabonde kukagua athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwashirikisha viongozi wa mitaa ili kwa pamoja watoe mapendekezo ya nini kifanyike kisha wampatie ripoti ya kuonyesha hatua za kukabiliana na Mafuriko ya Mara kwa Mara.*

Aidha *RC Makonda* amesema *athari zinazoonekana kwa sasa ni matokeo ya Jamii kuwafumbia macho watu wanovunja sheria kwa kujenga mabondeni, kuchimba mchanga na kuziba mikondo ya maji* jambo linalopelekea Mafuriko hivyo ametaka *kila mwananchi kuwa mlinzi wa mwenzake.*

Pamoja na hayo *RC Makonda* amesema kwa sasa *serikali inaendelea kurejesha miundombinu na madaraja yaliyochukuliwa na Mafuriko* ikiwemo ujenzi wa *madaraja ya muda mfupi* ili kuwezesha shughuli za kijamii kuendelea.

*RC Makonda* pia amewaelekeza *wakandarasi kutumia kipindi hiki cha mvua kuangalia kama Design ya madaraja wanayojenga yanakidhi kuhimili na kupitisha maji ya mvua ili wabuni design mpya zinazokidhi viwango.*

No comments