Ads

YANGA YAUWA MNYAMA TAIFA MBELE YA JPM NA RAIS WA CAF.

 
Na Mwamba wa habari
YANGA SC Imeodhihirisha ubabe wake  baada ya kuwachapa mahasimu wao wa jadi   Simba wekundu wa msimbazi bao 1-0 katika mechi ya ligi kuu iliyochezwaleo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

Mfungaji wa bao hilo alikuwa ni  mshambuliaji hatari  mwenyesifa ya kutembea juu ya mpira , Bernard Morrison aliyefunga bao hilo  dakika ya 44 kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 25.

Morrison, mchezaji wa zamani wa Heart of Lions, Ashanti Gold za kwao Ghana, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Delhi Dynamos FC ya India na Orlando Pirates ya Afrika Kusini alifunga bao hilo baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na kiungo Jonas Gerlad Mkude. 

Na Yanga walipata bao hilo baada ya beki tegemeo wa kati wa Simba SC, Erasto Edward Nyoni kuzidiwa  na kushindwa  kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Kennedy Juma Wilson dakika ya 23 .

Pamoja na Yanga kumaliza dakika 45 za kwanza ikiwa inaongoza, lakini ni Simba SC walijaribu kufurukuta japo hawakufua dafu  pamoja na kujaribu kutengeneza nafasi Yanga ilionekanakuwa  bora zaidi.

Aidha mlinda mlango, Metacha Boniphace Mnata alionekana bora zaidi kwa kuyafanya mashuti yasimba kuwa nyanya huku akisaidiwa na mabeki.

Kipindi cha pili Simba SC waliingia kichwa kichwa wakisaka bao lakini juhudi zao hazikuzaa matunda kwani mipango yao yote ilitibuliwa na mabeki na golikipa wa Yanga.
Mfungaji wa bao la Yanga, Morrison naye akashindwa kuendelea na mchezo , baada ya  kuumia  na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Sibomana.

Kwa sehemu kubwa ya kipindi cha pili, Yanga SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji Luc Eymael anayesadiwa na mzawa, Charles Boniface Mkwasa ilicheza kwa ilicheza kufa kupona na kuhakikisha inapata bao lapili lakini mipango hiyo haikufanikiwa kutokana na wapinzani wao kujihami kilawakati.

Dakika ya 70, kocha wa Simba SC, Mbelgiji pia Sven Ludwig Vandenbroeck anayesaidiwa na mzawa , Suleiman Matola alimpumzisha mshambuliaji wake wake wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere  baada ya kukosa mbinu za kuipenya ngome ya Yanga timu ya wananchi na kumuingiza kiungo Hassan Dilunga.

Simba  wekundu wa msimbazi wamepata kichapo hicho mbele ya  Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad, Rais wa TFF Walles Karia na   Mfadhili wao Mohamed ‘Mo’ Dewji pia Mwenyekiti wa klabu  ya Mabingwa hao wa kihistoria , Dk. Mshindo Msolla.  

Kwaushindi huo Yanga imefikisha pointi 50 baada ya ushindi wa leo katika mchezo wa 25 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya tatu, sasa ikizidiwa pointi moja Azam FC inayoshika nafasi ya pili ingawa imecheza mechi mbili zaidi.

Mabingwa watetezi, Simba SC wanaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa mbali, wakiwa na pointi 68 baada ya kucheza mechi 27.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa: Metacha Mnata, Juma Abdul, Jaffar Mohammed, Lamine Moro, Said Juma ‘Makapu’, Feisal Salum/Kelvin Yondan dk90+4, Papy Tshishimbi, Haruna Niyonzima, Bernard Morrison/Patrick Sibomana dk56, Ditram Nchimbi na Balama Mapinduzi/Deus Kaseke dk86.

Simba: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni/Kennedy Wilson dk23, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Luis Miquissone, Clatous Chama, Meddie Kagere/Hassan Dilunga dk70, John Bocco na Francis Kahata/Deo Kanda dk62.

No comments