TCRA yafikisha Kampeni ya Sirubuniki mjanja haingizwi chaka kwa viongozi wa Dini Morogoro.
Wameyasema hayo wakati wa Semina ya Kamati ya Amani ya Mkoa Morogoro inayotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutoa elimu juu ya utumiaji wa huduma za mawasiliano kwa kujinga na Uhalifu unapotumia huduma hizo.
TCRA ipo katika Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja ambayo inakwenda katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani katika kutoa elimu hiyo utumiaji wa huduma za mawasiliano.
Akizungumza katika Semina hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano wa Kamati ya Amani Mkoa wa Morogoro Juma Ng'ondavi amesema kupata Semina ya huduma za mawasiliano kuna umuhimu kutokana na wao wanazunguka jamii yote ya Mkoa huo.
Amesema kuwa Kazi yao ni pamoja kuwa mabalozi kwa viongozi ambao hawajafika kuendelea kutoa elimu katika ibada ili waumini waweze kupokea elimu ya kujikinga na uhalifu wakati unapotumia huduma za mawasiliano.
Katibu wa Makanisa Mkoa wa Morogoro na Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Mkoa huo Mchungaji Canon Regnald Mdugi amesema elimu waliopata TCRA wataipeleka kwa waumini kwa kuhakikisha wanaelewa katika kujikinga na uhalifu wakati kutumia mitandao ya mawasiliano.
Amesema viongozi wa dini kazi yetu ni kuitumia elimu hii na kuipeleka kwa waumini kwa ustawi wa nchi yetu
Kampeni ya kuelimisha jinsi ya kujikinga na uhalifu wakati wa kutumia huduma za mawasiliano ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Sirubiniki Mjanja haingizwi chaka inayolenga katika kuelimisha umma ya kujikinga.
Wakichangia katika semina hiyo viongozi hao wamepongeza juhudi za Mamlaka ya Mawasiliano za kuwalinda wateja na kuahidi kushiriki katika kampeni hiyo.
Kamati hiyo imetoa wito kwa taasisi kuiga mfano wa TCRA katika kuelimisha viongozi wa dini wanawafuasi wengi na ushawishi mkubwa katika jamii.
Kampeni ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka imeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano kushirikiana na Jeshi la polisi kitengo cha uhalifu mitandaoni yenye lengo la kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga ili wasirubuniwe wanapotumia huduma za mawasiliano.
Kampeni ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka inalenga kuzifikia kamati za Amani za mikoa yote ya Tanzania.
Kamati za Amani za mikoa ni kamati za viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali ambazo zimeundwa kwa lengo la kujenga maridhiano kwa watu wa dini mbalimbali
Nae Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Christopher John amesema kuwa viongozi wa dini ni watu mhimu sana katika kutoa elimu kwa waumini.
Amesema kuwa huduma za mawasiliano ni pana na teknolojia yake inabadilika kila siku
John amesema TCRA itaendelea kutoa elimu kuhusiana na matumizi ya Mawasiliano kuhakikisha yanakuwa salama kwa ustawi wa nchi.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa wanafikia makundi yote katika Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja.
Amesema wakati amefikia wa kutumia mawasiliano kwa kulinda usalama wa nchi pamoja na wanaotumia mawasiliano bila kufuata sheria na taratibu mkono wa sheria utawakuta.
Do you understand there's a 12 word phrase you can speak to your man... that will induce deep feelings of love and impulsive attraction to you buried within his heart?
ReplyDeleteBecause deep inside these 12 words is a "secret signal" that fuels a man's impulse to love, cherish and look after you with his entire heart...
12 Words Will Trigger A Man's Love Impulse
This impulse is so hardwired into a man's genetics that it will make him try better than ever before to take care of you.
In fact, triggering this mighty impulse is absolutely important to having the best possible relationship with your man that the instance you send your man a "Secret Signal"...
...You'll soon notice him expose his soul and mind for you in a way he's never expressed before and he will recognize you as the one and only woman in the galaxy who has ever truly attracted him.