WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA MWONGOZO WA KITAIFA WA TIBA YA MAGONJWA YA SARATANI
Na Maria Kaira,Mwambawahabari
WAZIRI wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amezindua mwongozo wa kitaifa wa Tiba ya magonjwa ya Saratani ambayo hurahisisha Mawasiliano kati ya madaktari bingwa na wataalamu wengine wa matibabu ya Saratani nchini.
Akizindua mwongozo huo jijini Dar es Salaam kuelekea siku ya maadhimisho ya Saratani Duniani, Waziri Ummy alisema mwongozo huo utarasisha uandaaji wa maiteo na ununuzi wa dawa katika vituo vya afya nchini.
Alisema faida ya mwongozo huo utawezesha wananchi kupata huduma Bora na viwango vya hali ya juu katika vituo vyote vya matibabu nchini kwa kuwa matibabu yote yatapangwa kwa kufuata mwongozo huo.
"Serikali kupitia Wizara hii itahakikisha mwongozo huu unasambazwa na kupatikana katika hospitali na Taasisi zote nchini ambayo itatoa matibabu ya Saratani na itafuatilia utekelezaji wake" alisema Ummy.
Licha ya uzinduzi wa mwongozo huo Waziri Ummy alitoa tamko kuhusu mwendo wa Saratani nchini ambapo alisema Ugonjwa wa Saratani unakua kwa kiasi kikubwa.
Kwa Mujibu wa za Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani IARC na Shirika la Afya Duniani( WHO) mwaka 2018 zinaeleza kuwa wagonjwa wapya wa Saratani wanakadiriwa kufikia milioni 18.1na Kati yao zaidi ya wagonjwa 9.6 hufariki kutokana na Ugonjwa huo.
Alisemà Saratani limekuwa likiongezeka na kukua siku hadi siku ambapo Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya 42,060 kwa mwaka na takribani wagonjwa 28,610 hufariki kwa mwaka sawa na asilimia 68.
Pia kwa mwaka 2019 takwimu kutoka hospitali zinazohudumia wagonjwa wa Saratani zinaeleza kuwa wagonjwa wapya zaidi ya wagonjwa 13,215 sawa na asilimia 31 walipatiwa matibabu.
"Hivyo tunawahimiza wagonjwa wote wanaohisiwa kuwa na Saratani nchini wafike katika hospitali ili wapate uchunguzi wa tiba sahihi" alisisitiza Ummy.
Hata hivyo mwaka 2019 hospitali za Ocean Road 7,789, Bugando1687, KCMC 983, Muhimbili 1437 , hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya 319 na wagonjwa wengine 1000 kutoka hospitali binafsi ya Hindu Mandal, Kairuki na vituo mbalimbali vya mikoani.
Naye Mkurugenzi WA Taasisi ya saratani ya Ocean road Dk.Julius Mwaiselage amesema taarifa kutokaTaasisi ya Saratani ya Ocean Road hapa nchini mwaka 2019 zinaonesha aina za Saratani zinazoongoza kwa wanaume na wanawake .
Upande wa wanaume Saratani inayoongoza ni Tezi dume kwa asilimia (23) Saratani ya Koo la chakula asilimia (16) Saratani ya kichwa asilimia (12) Saratani ta utumbo mkumbwa na mdogo asilimia (11.4)
Kwa upande wa wanawake Saratani inayoongoza ni Saratani ya mlango wa kizazi kwa asilimia (47)ikifuatiwa na Sarati ya Matiti asilimia (16) Saratani ya utumbo mkumbwa na mdogo asilimia (5.8)na Saratani ya Koo asilimia (5.3)
Hata hivyo Waziri Ummy ametoa wito kwa watanzania kuwa na tabia ya kupima Afya Mara kwa Mara ili kuweza kugundua tatizo la kiafya mapema na kuweza kupata tiba kwa wakati.

Post a Comment