WAZIRI KAIRUKI AZINDUA KONGAMANO NA MWONGOZO WA UWEKEZAJI SONGWE
Mwambawahabari
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Uwekezaji Angella Kairuki mapema leo amezindua Kongamano na
Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Songwe huku akiwahakikishia washiriki wa
Kongamano hilo kuwa Mkoa wa Songwe ni mahali salama kwa uwekezeji.
Waziri Kairuki amesema
Songwe ina fursa za uwekezaji na biashara ndani ya Mkoa lakini pia ina nafasi
kipekee ya Kimkakati iliyonayo kwakuwa ni Lango Kuu la SADC na hivyo kuwa
kiungo cha kibicashara kati ya Tanzania na Nchi 6 kati ya 16 za SADC.
“Ni matumaini yangu kuwa
kaulimbiu ya Songwe Lango la SADC itaenda sambamba na kuhamasisha biashara kati
ya Mkoa wa Songwe na Mikoa ya jirani, lakini pia biashara baina ya Mikoa ya
jirani na Nchi za SADC kupitia Mkoa huu wa Songwe, Wekeni mikakati mizuri ya
kufanikisha hili.”, amesisitiza Waziri Kairuki.
Ameongeza kuwa Mwongozo wa
Uwekezaji aliouzinduaumebainisha kwa undani fursa nyingi za uwekezaji zilizopo Mkoa wa Songwe ikiwa ni pamoja na
Kilimo, Mifugo, madini, utalii na uhifadhi wa Misitu, na kuwa fursa zote hizi zinaufanya Songwe kuwa eneo
zuri la kuvutia wawekezaji.
Waziri Kairuki ametumia
nafasi hiyo pia kukumbushia maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa Mikoa ambayo bado haijaandaa Mwongozo wa Uwekezaji kufanye hivyo
mapema huku akiupongeza uongozi wa Mkoa wa Songwe kwa kuwapokea vizuri
wawekezaji kwakuwa hajawahi kupokea malalamiko yoyote kutoka kwa wawekezaji.
Pia ametoa rai kwa
Halmashauri zote nchini kukamilisha mchakato wa kutenga ardhi katika maeneo yao
kwa ajili ya uwekezaji na kuyawekea miundombinu stahiki ya msingi huku
akielezea kuwa eneo linaweza kuwa dogo ila lenye miundombinu ya kuvutia
wawekezaji.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amesema Mkoa wa Songwe unazo sifa nyingi
za kuwavutia wawekezaji ikiwa ni pamoja na halmashauri zote tano kutenga maeneo
ya Uwekezaji.
Brig. Jen. Mwangela
amesema Mkoa wa Songwe unavutia wawekezaji katika kilimo cha kisasa cha
Umwagiliaji kwakuwa hali ya hewa inaruhusu na kuna eneo la hekta 18,464 linalo
faa kwa kilimo cha Mbogamboga na matunda huku kukiwa na miundombinu ya barabara
na usafiri wa anga ili kuwezesha kusafirisha bidhaa hizo katika masoko ya ndani
na nje ya nchi.
Amezitaja fursa nyingine
ni uwekezaji katika Kilimo cha Mbegu, Usambazaji wa pembejeo na Zana za Kilimo,
fursa ya mitambo ya kukaushia mazao, fursa ya kuanzisha Ranchi, fursa ya mashamba
ya kutotoleshea vifaranga, fursa katika utalii kwenye maeneo ya utalii wa uwindaji, fursa ya makampuni ya kuongoza
watalii na kujenga hoteli za kitalii na Campsites.
Brig. Jen. Mwangela
amesema matarajio ya Mkoa ni kuwa baada ya Kongamano hilo wawekezaji
watapatikana katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Kwa upande wake Katibu
Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila amesema Takwimu za Mamlaka ya Mapato
Nchini (TRA) zinaonyesha kuwa alisilimia 70 ya mizigo inayotoka bandari ya Dar
Es Salaam kuelekea nchi za SADC huzifikia nchi hizo hupitia mpaka wa Tunduma
uliopo Mkoani Songwe.
Kafulila amefafanua kuwa
hiyo ni fursa kubwa kwa wawekezaji kwani wanaweza kujenga maeneo ya kutunzia
bidhaa, maegesho, bandari kavu na bandari huru katika Mkoa wa Songwe ambapo kwa
sasa fursa hizo bado hazija tumiwa vizuri.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Kampuni ya Shanta Gold Mine Roman Urasa amesema fursa ambayo Mkoa wa Songwe ya
kuwa Lango la SADC isiishie kuwa njia tu
ya bidhaa kwenda ya nchi jirani bali
Songwe izalishe bidhaa za kusafirisha nje ya nchi.

Post a Comment