WANANCHI WAFURAHIA KUFUNGULIWA KWA OFISI YA TRA KILOLO
Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi Bi. Rose Mahendeka kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) akiwaelimisha wananchi na wafanyabiashara (hawapo pichani) wa
Kata ya Dabaga Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kuhusu masuala mbalimbali
yanayohusu kodi wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea kufanyika
mkoani humo. Kampeni hiyo inatarajiwa kumalizika tarehe 22 Februari, 2020.
Na
Veronica Kazimoto
Kilolo
Wananchi na wafanyabiashara wa Wilaya ya Kilolo
mkoani Iringa wamefurahia kitendo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufungua
ofisi wilayani humo na kusema kuwa, uwepo wa ofisi hiyo siyo tu umewasogezea huduma
karibu bali utaongeza tija katika ukusanyaji mapato ya Serikali.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea mkoani humo,
wananchi hao wamesema kuwa, awali walikuwa wakisafiri umbali mrefu kwenda
Iringa mjini kufuata huduma za TRA suala lililopelekea kutumia muda mwingi tofauti
na ilivyo hivi sasa.
Prosper Mwinu ni
mfanyabiashara wa duka la vipodozi wilayani humo ambaye ameeleza kuwa ufunguzi wa
ofisi hiyo pia umewaondolea gharama walizokuwa wakizitumia kufuata huduma za
TRA Iringa mjini.
“Kwakweli tunaishukuru Mamlaka
ya Mapato Tanzania kutusogezea huduma karibu kwa kutufungulia Ofisi ya TRA hapa
Kilolo maana tulikuwa tunatumia gharama za kusafiri kwenda Iringa mjini kuifuata
TRA na wakati mwingine tulikuwa tunaingia gharama za kulala huko ikitokea
tumeshindwa kupata huduma zote kwa siku moja,” alisema Mwinu.
Naye, Grace Barnaba mfanyabiashara
wa duka la pembejeo alisema kwamba, wananchi wanapokuwa wamesogezewa huduma karibu
wanakosa sababu ya kutokulipa kodi kwa wakati kwani hawakutani na foleni na
hupata huduma hizo kwa haraka.
“TRA wamefanya jambo jema sana
kutufungulia ofisi hapa wilayani yaani hatuna tena sababu ya kuchelewa kulipa
kodi maana mwanzoni tulikuwa tunakutana na foleni kubwa Iringa mjini lakini kwa
sasa tatizo hilo limekwisha na tutalipa kodi zetu kwa wakati,” alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya
hiyo Bi. Asiah Abdallah amesema kuwa, ufunguzi wa Ofisi ya TRA wilayani kwake,
umewafurahisha sana wananchi kwa sababu walikuwa wakitembea umbali mrefu zaidi
ya kilomita 60 kwenda kutafuta huduma za kulipa kodi, hivyo ofisi hiyo mpya itawarahisishia
wananchi hao suala zima la ulipaji kodi na hatimaye kuongeza uchumi wa wilayani
hiyo.
“Kwahiyo ninachotaka kusema ni
kwamba, tumepiga hatua kubwa sana kuwepo kwa Ofisi ya Mapato katika wilaya yetu
ya Kilolo na hivyo tunategemea uchumi wa wilaya yetu utaongezeka kutokana na
kwamba wananchi sasa watakuwa wanalipa mapato katika njia ambayo ni rafiki na
rahisi”, alieleza Mkuu wa wilaya hiyo.
Kampeni ya elimu kwa mlipakodi
inayoendelea mkoani Iringa ilianza tarehe 17 na inatarajia kumalizika tarehe 22
Februari, 2020 ikiwa na lengo la kuwaelimisha wafanyabiashara na wananchi kwa
ujumla masuala mbalimbali yanayohusu kodi ikiwa ni pamoja na kupokea maoni yao,
mrejesho na changamoto za ulipaji kodi walizonazo ili kuzitafutia ufumbuz
Post a Comment