THBUB, LHRC wajipanga kutoa elimu ya haki za binadamu mashuleni.
Mwambawahabari
Na Mbaraka Kambona,
Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) na Kituo cha Sheria na Haki
za Binadamu (LHRC) wamekubaliana kuandaa mpango wa pamoja wa kutoa
elimu mashuleni ili kuhamasisha na kukuza haki za binadamu
nchini.
Makubaliano
hayo yalifikiwa na pande zote mbili baada ya majadiliano yaliyofanyika
katika kikao kilichowakutanisha ujumbe wa THBUB na Viongozi wa LHRC
kwenye ofisi za kituo hicho jijini Dodoma leo.
Akiongea
katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma, Mafunzo, Utafiti na
Nyaraka wa THBUB, Alexander Hassan alisema kuwa ili ushirikiano wa THBUB
na LHRC uwe na tija ni vyema kuunganisha nguvu katika maeneo
wanayofanya kazi zinazofanana.
Alexander
alisema kwakuwa taasisi zote mbili zimeanzisha Klabu za haki za
binadamu mashuleni ni vyema kuunganisha nguvu katika maeneo hayo ili
kupata matokeo makubwa zaidi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa LHRC, Anna Henga akichangia hoja hiyo alisema kuwa suala
hilo la kuunganisha nguvu ni zuri na ni muhimu likafanyiwa kazi kwa
haraka na kama uongozi wa THBUB utaridhia basi maafisa wa pande zote
mbili wakutane mapema iwezekanavyo ili kuandaa mpango huo.
Henga
alisema kuwa LHRC kwa muda mrefu imekuwa ikitoa elimu kwa umma kuhusu
masuala ya haki za binadamu kwa njia mbalimbali ikiwemo matumizi ya
vyombo vya habari, vipeperushi na mikutano ya hadhara na hivyo kuwafikia
watu wengi lakini ni muhimu kwa sasa kuunganisha nguvu na THBUB ili
kuepuka kutawanya nguvu na rasilimali kwa mambo ambayo wanaweza kufanya
kwa pamoja.
Henga
alisema kuwa wamefurahishwa na kuteuliwa kwa Makamishna wa THBUB kwani
kutasaidia wananchi kupata haki zao na ushirikiano wa wadau utaimarika
zaidi.
Alisema
kwa kuanza mpango huo itakuwa vyema kama watashirikiana kwa pamoja
kuimarisha elimu ya haki za binadamu katika klabu za mashuleni kwani
wakifanikiwa kuelimisha watoto shuleni wataweza kusimama na kutetea haki
zao wenyewe.
Mwenyekiti
wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu alisema katika kikao hicho kuwa
THBUB inatambua mchango mkubwa wa LHRC katika kukuza na kutetea haki za
binadamu na alimuhakikishia Mkurugenzi wa kituo hicho kuwa tume
itaendelea kushirikiana kwa karibu na kituo hicho kwa kuwa wote lengo
lao ni kusaidia wananchi kupata haki zao.
Aidha,
alisisitiza kuwa katika kutekeleza majukumu yao ni vyema kujikita
kusaidia jamii na serikali kwa ujumla kutekeleza majukumu yake, pale
ambapo serikali inafanya vizuri ni vyema kupongeza na pale inapoonekana
imekosea basi ni vyema kutafuta namna nzuri ya kukosoa
Post a Comment