KIGWANGALLA ACHANGISHA MILION 117 ZA HARAMBE KITUO CHA AFYA
WAZIRI wa Mariasili na Utalii Dkt. Khamis Kigwangala amechangisha shilingi milioni 117 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha afya Ketumbeine Wilayani Longido.
Akiongoza harambee hiyo mwishoni mwa wiki Waziri Kigwangala alisema afya ni muhimu kwa maisha ya mwanadamu ndio maana tumevuka lengo lililokusudiwa lengo lilikuwa shilingi milioni 100.
Waziri Kigwangala alisema harambee hiyo imehusisha wananchi wa eneo hilo wa kabila la Masai ,ambapo Mbunge wa Jimbo hilo Dkt. Steven Kiruswa ,viongozi wa halmashauri ya Longido ,mashirika, wadau wa maendeleo na taasisi za hifadhi zilizo chini ya Wizara ya Mariasili na utalii .
Akizungumza wakati wa harambee hiyo Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangala ambaye alikua mgeni rasmi amewapongeza wananchi wa Kata hiyo kwa kujitolea na kuwataka waendelee kushiriki na kuunga mkono miradi mbalimbali ya maendeleo inayoanzishwa na kutekelezwa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais, Dkt.John Magufuli.
Dkt. Kigwangalla amewaeleza wananchi hao kuwa Serikali ya awamu ya tano imekua ikitekeleza na kukamilisha kwa vitendo miradi mbalimbali ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, miradi ya maji, umeme na huduma za afya, elimu.

Post a Comment