Ads

MANISPAA YA ILALA WAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BILIONI 181.7





Meya wa Halmashauri ya Ilala Leo January 28 /2020 ameongoza kikao cha Baraza la Madiwani la manispaa ya Ilala ambapo Katika Baraza hilo madiwani wa Ilala wamepitisha bajeti ya shilingi bilioni 181 (Kulia) Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Elizabeth Thomas. (PICHA NA HERI SHAABAN)

MANISPAA ya Ilala   imepitisha bajeti ya Sh.bilioni 181.7 kwa mwaka wa fedha 2020//2021.

Bajeti hiyo ilipitishwa jana katika kikao cha Baraza la Madiwani lililokuwa linajadili makadirio ya Mapato na matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2020/2021.

Akitoa taarifa ya mikakati hiyo, Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Ojambi Masaburi alisema Kati ya fedha hizo Sh.bilioni 6o ni fedha kutoka vyanzo vya ndani na Sh.bilionii 121.7 ni kutoka ruzuku ya Serikali Kuu.

"Bajeti ya Mapato ya ndani imeongezeka kwa asilimia tano ikilinganishwa na bajeti ya zaidi ya Shilingi bilioni 57 ya mwaka 2019/2020 ambayo imesabaishwa na ongezeko la gharama za uchangiaji huduma za afya pamoja na kuongezeka vituo vitano vya afya,"alisema Masaburi 

Naibu Meya Masaburi aivitaja vituo hivyo kuwa ni Hospitali ya Wilaya ya Kivule, Zahanati ya Mbondole, Luhanga, Bangulo na Linakata.

Kwa upande wake Mchumi wa Manispaa Ilala Mangiwa Kiganomo alisema katika bajeti ya mwaka 2020/2021 halmashauri ya Ilala kupitia Kamati ya mipango miji na Mazingira imepanga kutumia zaidi ya Sh.bilioni 26 Kati ya hizo Sh.bilioni Saba ni fedha za ndani za halmashauri na Sh.bilioni 18.2 ni kutoka Benki ya Dunia kupitia mradi wa Maendeleo wa DMDP.

 Mchumi Mangiwa  alisema miradi ya maendeleo itakayotekelezwa katika Kamati ya mipango miji na Mazingira kwa mwaka 2020/2021 ni pamoja na ujenzi wa kituo cha mabasi katika eneo la Chanika, ununuzi wa mafuta ya greda kwa ajili ya uchongaji wa Barabara kwenye kata 36 za Manispaa na ununuzi wa vifusi kwa ajili ya barabara kwenye kata 36 za Manispaa.

Meya wa Manispaaa ya Ilala Omary Kumbilamoto   alisema bajeti hiyo imelenga kukamilisha miradi yote ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa,ukamilishaji Barabara Kimanga _ Mazda (1.0 km), kwa kiwango cha lami kazi husimamiwa na Wakala wa Barabara Vijijini (Tarura) , uhamasishaji na ujengaji wa mfereji wa maji ya mvua ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), katika eneo la Kalakata na Tazara.

Pia Idara ya maji na udhibiti wa maji Taka, ardhi na makazi, usafi na mazingira, Kitengo cha nyuki.

Meya Kumbilamoto alisema, ushirikiano baina ya madiwani, wafanyabiashara na watendaji wa Manispaa hiyo umesaidia kuongeza Mapato ambapo awali walikuwa wanakusanya bilioni 57 hivi sasa imefikia Sh.bilioni 60.

" Kwa mwaka huu wa fedha tunatarajia kufanya vizuri zaidi katika ukusanyaji Mapato kwa kutumia vyanzo vyetu vya Mapato vya ndani,"alisema kumbilamoto

No comments