Ads

MBUNIFU MASHINE YA MAFUTA AELEZA JINSI WAKENYA WALIVYO CHANGAMKIA MAFUTA YA PARACHICHI



Na John Luhende
Mwamba wa habari
Imeelezwa kuwa wananchi nchini Kenya wamekuwa wakitumia mafauta ya parachichi kwa wingi ukilinganisha na Watanzania ambako ndiko mafuta haya yanatengenezwa kwa wingi.

Hayo yameelezwa naJesse Oljange , Mkurugenzi wa kampuni ya Avomeru Oil inayotengeza mafutahayo alipo kuwa katika maonesho ya badhaa za viwanda zinazozalishwa hapa nchini ambapo amesema mafuta hayo ni bora kwa afya ya binadamu na hayana kemikali na kwamba wakenya wameyapenda kwa kuwa hayana madhara .

"Tunayatengeneza hapa nchini kwetu lakini kiukweli soko letu kubwa ni nchini Kenya nawaomba watanzania wayaamini mafuta haya na mimi nime kuja hapa katika maonesho ili kuwapa elimu watanzania kuhusu mafuta haya wayatumie kama kipodozi hayana madhara wenzao Kenya wamegundua napia tumekuwa tukiwauzia wenye viwanda kama malighafi "Amesema .

Alisema wkati anafikiria kufanya kazi hiyo hakufikiria kuhusu kupata fedha alikuwa anataka kuwa saidia wakulima ambao wana matunda ya parachichi kwani yalikuwa yanaoza kwa wingi na sasa teknolojia hiyo imewasaidia wakulima hawapotezi tena matunda yao wanafaidika na kilimo hicho.

Pamoja na hayo ametoa wito kwa watanzania kutojikita tu katika mambo ambayo ni makubwa kama utalii na madini ,kunafaida kubwa sana katika usindikaji wa mazao na shukuru Serikali kwa kutuwezesha kupita COSTECH lakini nawaomba waongeze nguvu zaidi katika kuendeleza hizi teknolojia ndogo zinazo buniwa na watanzanzania.

Naye kaimu afisa habari wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Deusidedith Leonard amesema ,Tume hiyo imekuwa ikiwasaidia wabunifu kuhifadhi na kuendeleza bunifu zao na baada ya kuona mbunifu wa teknolojia hii anatumia vifaa duni , COSTECH ilimuwezesha kumendeleza kwa kumpatia vifaa vya kuendeleza teknolojia yake.

"Nawaomba watanzania tuwaunge mkono vijana wetu kwa kununua bidhaa wanazo zitengeneza wanabidhaa zenye ubora na viwango vya kimataifa"Alisema.

Alimaliza kwakusema kuwa Serikali kupitia  COSTECH ,imekuwa msaada mkubwa kwa wabunifu pamoja na kuwapa msaada wa kifehda wameendelea kuwapa elimu ya kulinda bunifu zao tofauti na hapo awali walikuuwa wakipoteza milikwa wakienda katika maonesho kama haya wanaeleza kila kitu halafu baadaya muda unakuta mtu mwingine anawahi kusajili kutengeneza na kuingia sokoni .

 

No comments