Ads

WASANII WA FILAMU WATAKIWA KUSOMA RASIMU KATIBA YAO, KUTOA MAONI.




RAIS wa shirikisho la Filamu nchini Simon Mwakifwamba amewataka wadau na wasanii katika sekta ya Filamu nchini kupitia rasimu ya katiba ya shirikisho hilo ili kuweza kutoa maoni yao kwa lengo la kupata katiba itakayoongoza shirikisho.


Anasema shirikisho baada ya kubaini uwepo wa changamoto mbalimbali katika katika katiba ya awali na ili kwenda na wakati uliopo waliamua kuazisha mchakato wa kupata katiba mpya ambapo rasimu yake imeshabalikiwa na vyombo mbalimbali hivyo ni nafasi kwa wadau kutoa maoni yao.

 Mwakifywamba aliyasema hayo jana jijini Dar Es Salaam katika mkutano na waandishi wa Habari ambao pia uliweza kushirikiana viongozi Kutoka Basata,Bodi ya Filamu Tanzania ,na wadau wengine wa tasnia hiyo.

 Mwakifwamba alisema  shirikisho hilo liliazishwa na wadau wa tasinia ya Filamu Tanzania  ambayo imepewa mamlaka ya kusimamia tasinia ya Sanaa nchini namba 4 ya mwaka 1984 .

 Pia alisema TAFF inashirikiana na taasisi ya Serikali ,Bodi ya Filamu Tanzania ambayo imepewa mamlaka ya kuisimamia tasnia ya Filamu Tanzania  kwa Sheria namba 4 ya mwaka 1976.

 "Mambo makuu ambayo shirikisho la filamu Tanzania linayasimamia kwa mujibu wa makubaliano yake na BASATA ni kufanya uzengezi ,kufanya utetezi  na pia kueneza AMA kusaidia elimu kwa watu wake." Alisema

 Alisema katika maeneo hayo ya utendaji maeneo ya utendaji kazi wake wadau inaowasimamia TAFF imefanikiwa kwa kiasi chake na pia kama taasisi inayoendelea kukomaa inakumbana na changamoto kadhaa.

 Mwakifwamba alisema wamajivunia ni pamoja na kupigania sera ya Filamu Tanzania tangu mwaka 2014 na Serikali imeshaitoa ahadi kwamba kabla ya mwaka huu haujaisha itakuwa tayari imeishapatikana na pia kama mdau muhimu wa sekta ya Sanaa bunifu nchini imehakikisha kuwa msimamizi Mkuu wa maendeleo ya tasinia ya Filamu Tanzania ambaye ni bodi ya inakua na uongozi imara kama ilivyo sasa.

 Pia alisema pamoja na yote TASS imekuwa mstari wa mbele kupaza sauti kubwa kwaniaba ya wadau inaowangoza pindi inapohitajika.

 Kuhusu Changamoto alisema imekuwa ikikumbwa na  ukata wa kifedha ambao.mara kadhaa inashindwa kuyashugulikia masuala yake ya kiongozi na ya tasnia inavyotakiwa .pia migogoro ya mara kwa Mara nayo imekuwa  ikiliyumbisha shirikisho la filamu Tanzania na vyama vyake ambavyo vipo kumi.

Alifafanua kuwa migogoro hiyo ndio iliyopelekea Bodi ya filamu Tanzania kupitia kwa Mwenyekiti wake Profesa Frowin Nyoni kuitisha kikao na wadau wa tasnia ya Filamu walio katika uongozi wa shirikisho na vyama vyake kujadili namna bora ya kuitatua migogoro hiyo ambapo inaonekana kuwa tatizo kuu ni kukosekana kwa mifumo thabiti wa uongozi unaoweza kusaidia viongozi na wanaongozwa kutenda kazi kwa mujibu wa taratibu zilizopo.

 Alisema Kutoka na hali hiyo ndipo Serikali na wadau wa Filamu Tanzania pamoja na Bodi ilikaa na kuazimia kwa pamoja kuundwa kwa katiba mpya ya kuliongoza shirikisho na rasimu hiyo ya katiba iliundwa na kupelekea wadau wake kupitia kwa vyama wanachama kitaifa lakini baada ya kikao cha tathimini ya utendaji kazi kati ya bodi ya Filamu Tanzania.

 Alisema wameazimia mchakato huo wa ukusanyaji maoni utakuwa wa muda wa mwezi mmoja tu .rasimu zitapatikana kupitia njia mbalimbali ikiwamo mitandao ya kijamii ,face book, whatsapp ,magazeti, blogs.na Mara baada ya upokeaji maoni kukamilika shirikisho kupitia kikao chake cha bodi itaitisha mkutano Mkuu wa wanachama wake kwa ajili ya agenda kuu moja ya kujadili kisha kuipitisha ama kuikataa rasimu hiyo pendekezwa.

 "Tutasambaza ofisi zote za maofisa utamaduni popote walipo na hivyo wadau wengine waende huko ili kupata kopi hizo na wakishatoa.maoni yao warudishe hapohapo ofisini ." alisema Mwakigwamba

 Kwaupande wake Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mwingereza alisema jambo ambalo wanalifanya shirikisho hilo nikutaka kwenda na wakati na kushindwa kwenda na wakati ni kutokwenda na wakati.

 Alisema kutokana na hilo wanalolifanya ni jambo jema na anawapongeza shirikisho kwa kazi hiyo na hasa katika umuhimu wa kushirikiana wadau na wasanii wenyewe hivyo kama Basata wanapongeza.

 Mwingereza alisema sekta hiyo ya Filamu inakua kwa.kasi zaidi kwa asilimia 13.7 hivyo kuna haja ya.mashirikisho mengine kuiga yanayofanywa na shirikisho na kuwataka wengine kuboresha katiba zao ili kwenda na wakati.

 Naye Kaimu  Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania  Dkt Kiagho Kilonzo alisema nafasi yao ni kusukuma pale ambapo walikwama shirikisho ili kuweza kufikia mwisho.

 Alisema katiba ilikuwa ni Kero kwa wadau pamoja na wasanii hivyo ndio.maana wameweza kufanya yaliyofanyika ili kuweza kupata katiba itakayoweza kuongoza shirikisho la bodi ya Filamu nchini.

Aliwataka wadau kutoa maoni yao ili kuweza kupata katiba hiyo ya shirikisho.

No comments