Ads

MITAMBO YA KUNYANYULIA MIZIGO YA UJENZI WA MRADI WA JN HPP YAZINDULIWA RASMI FUGA

Mwambawahabari
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye(wa pili kutoka kushoto) akiambatana na Msemaji Mkuu wa Serikali,Dkt.Hassan Abbasi (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi mtendaji wa TAZARA-Zambia, Mhandisi.Bruno Chingandu (wa kwanza kulia) na Meneja wa TAZARA ,Mkoa wa Tanzania, Fuadi Abdallah wa pili kulia wakiwa katika uzinduzi wa  mitambo ya kunyanyulia mizigo stesheni ya Fuga.


 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye(wa pili kutoka kushoto) akivaa kofia kujiandaa kuwasha moja ya mitambo ya kunyanyulia mizigo ya ujenzi wa mradi wa Umeme JN HPP iliyopo katika Stesheni ya Fuga, wa kwanza kushoto ni Meneja wa TAZARA ,Mkoa wa Tanzania, Fuadi Abdallah.


 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akiendesha  moja ya mitambo  ya  Kunyanyulia mizigo iliyoko katika stesheni ya Fuga wakati wa ufunguzi wa  mitambo hiyo hapo jana Agosti 19, 2019.

 Wafanyakazi wa Stesheni ya Fuga wakishuhudia uwezo wa  mtambo aina ya Raech Stacker wa kunyanyua mizigo mizito  katika stesheni ya Fuga uliozinduliwa jana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye.


 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akitelemka kutoka kwenye moja ya mtambo wa kunyanyulia mizigo  mara maada ya kuuzindua hapo jana katika Stesheni ya Fuga itayotumika kopokea na kusafirisha mizigo kwenda  mradi wa Umeme JN HPP.



 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akipata maelezo fulani kutoka kwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi wakati wa uzinduzi wa mitambo ya kunyanyulia mizigo ya ujenzi wa mradi wa umeme JN HPP uliofanyika katika Stesheni ya Fuga.



(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)

No comments