MABARAZA YA ARDHI KIGAMBONI YATAKIWA KUZALISHA MAPATO.
Mwambawahabari
Na. John
Luhende
Ufafanuzi
kuhusu utaratibu wa Mabaraza ya Ardhi ya
kata umetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni
Ludigija Ng’wilabuzu, kutokana na
malalamiko ya wananchi kuhusu mabaraza hayo kuwa yamegubikwa na Rushwa jambo
ambalolimesababisha usumbufu kwa wananchi.
Madai
hayo yameibuliwa na diwani wakata ya Mjimwema, Celestine Maufi , wakati akiuliza swali la
papo kwa papo katika kikao cha baraza la madiwani robo ya pili ambapo
amesema wajumbe wa baraza hilo wamekuwa
wakiombaomba fedha kwa Madiwani jambo
ambalo pia linalalamikiwa na wananchi kuwa kumekuwa na vitendo vya rushwa.
‘’Wajumbe
hawa hawalipwi posho wala mishahara hali hii imasababisha kuomba rushwa kwa
wananchi wanao hudumiwa na mabaraza
naomba kama kuna uwezekano wa
kulipwa basi walipwe rushwa imezidi ”Alisema
Maufi
Akijibu
swali hilo Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni,
Ludigija Ng’wilabuzu, amesema
yeyote atakeye kamatwa akipokea amakutoa rushwa atachukuliwa hatua za
kisheria , na akafafanua kuhusuhu malipo
ya wajumbe hao amesema .
“Kwa maana
ya utaratibu Mabaraza haya yanatakiwa
yakusanye fedha na yakikusanya tunatakiwa tuwarudishie asilimia 80% au kadri
itakavyo kuwa imeelekezwa katika miongozo lakini sasa imekuwa ni vigumu
kuwalipa na nimesha kutana nao mara
nyingi hawaleti chochote sasa tunawezaje kumlipa mtu ambaye hazalishi?
Wanakusanya fedha nyingisana lakini hawawasilishi tumeana andaa utaratibu tutakutana nao tuwaelekeze “Alisema
Aidha
kumetolewa ushauri wa ujenzi wa miradi
ya kimkakati ilikuleta tija itakayo
iwezesha Manispaa ya Kigamboni Kujiendesha
badala ya miradi hiyo kujengwa maeneo
ambayo sirafiki kibiashara, Diwani wa kata ya Vijibweni ambaye pia ni Meya wa jiji la Dar es salaam, Isaya
Mwita , ameshauri miradi hiyo kujengwa
sehemu yenye mkusanyika wa watu wengi na inayofikika kirahisi kimiundo mbinu mfano
soko badala ya kujengwa kibada lijengwe
Fery ,kwa msomari au vijibweni.
“Sina maana
kuwa mbadilishe lakini nashauri mnaweza
kufanya ( review) mapitio ,miradi hii tuwe nayo makini tujenge maeneo ambayo kunamzuguko wa biashara na ambapo hata watu
kutoka maeneo ya jirani kama kurasini wanaweza kuja kupata mahitaji , masoko kama sterio ya
Temeke yako katikati yanafikika Kirahisi.
Hata hiyo
Naibu Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mzuri Sambo,
ametetea hatua ya kujengwa soko la kimkakati katika kata ya Kibada
akisema kuwa soko hilo litatumiwa na wanakibada hata kama hawata weza watu
wengine kufika huko.
‘’mimi
nasema kwenye kata yangu tuko vizuri
soko hilo tutalitumia, hatutegemei watu kutoka nje huko unakosema wanakibada wenyewe tunatosha , pia nashauri tuibue
maeneo na tuyathibitishe Manispaa yapae
hati tupewe na mhe.Rais anasema anazo fedha ila watu wakuzitumia hawapo hana hel
ya kuchezea “Alisema Sambo


Post a Comment