Mahakamani leo Katika Kesi ya Zitto Kabwe na Spika Ndugai

Kesi ya Zitto Vs. Spika Ndugai kuomba tafsiri ya Mahakama kuhusu madaraka ya Bunge kumuita na kumuhoji CAG (Miscellaneous Civil Cause No. 1/2019) imeahirishwa hadi Februari 15 itapoitwa tena kwa ajili ya kusikilizwa
Kesi
hiyo ya Kikatiba imefunguliwa Mahakama Kuu na mbunge wa Kigoma Mjini
(ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe dhidi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Katika
kesi hiyo, Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa ACT anaiomba Mahakama Kuu
itoe tafsiri ya kinga ya CAG, Profesa Mussa Assad iliyopo kikatiba na
pia kutoa tafsiri ya Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge katika
kushtaki watu wanaosemekana kulidharau Bunge.
Kesi
hiyo inayosikilizwa na jopo la majaji watatu; Firmin Matogolo (kiongozi
wa jopo), Dk Benhajj Masoud na Elinaza Luvanda imetajwa leo Alhamisi
Januari 31, 2019 kwa mara ya kwanza mahakamani hapo na mahakama hiyo
ikapanga kuanza kuisikiliza rasmi Februari 15, 2019.
Pia,
mahakama hiyo leo imewaamuru wadaiwa (Spika na AG) kuwasilisha
mahakamani hapo utetezi wao ndani ya siku 14, ambazo zinaishia Februari
13, 2019.
Wakati
kesi hiyo ilipotajwa leo, Zitto hakuwepo mahakamani na aliwakilishwa na
wakili wake, Fatma Karume huku Ndugai akiwakilishwa na jopo la
mawakili watatu wa Serikali, wakiongozwa na mwanasheria wa Serikali Mkuu
(PSA), Alesia Mbuya.
Zitto
alifungua kesi hiyo baada ya Ndugai kupitia kwenye vyombo vya habari na
baadaye kumwandikia barua CAG akimtaka afike mbele ya kamati hiyo ya
Bunge kuhojiwa kutoka na kauli yake aliyoitoa akiwa anahojiwa na Idhaa
ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kuwa Bunge la Tanzania ni dhaifu.
Post a Comment