Mawaziri wakutana Mbeya kumpongeza Rais Magufuli
Mawaziri wameungana kumpongeza Rais John Magufuli kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini kwa kasi kubwa.
Pongezi
hizo zimetolewa leo Jumamosi Desemba 29, 2018 jijini Mbeya katika
kongamano la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT)
lililofanyika kitaifa jijini humo.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema Rais
Magufuli amefanya kazi kubwa kuhakikisha elimu inapatikana kwa wote bila
kujali hali zao kiuchumi.
"Mheshimiwa
Rais ameweza kusaidia kutolewa kwa elimu bure jambo lililopelekea
ongezeko la watoto wanaoandikishwa katika shule zetu," amesema Profesa
Ndalichako.
Naye
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angellina Mabula
amesema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli imesaidia kwa
kiasi kikubwa kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi.
"Serikali inaandaa mfumo ambao utasaidia kuondokana na tatizo la ardhi kumilikiwa na mtu zaidi ya mmoja," amesema Mabula.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso amesema miradi
iliyotakiwa kutekelezwa katika awamu hii ni 1,810 lakini mpaka sasa
miradi 1,659 imekwisha kutekelezwa.
Post a Comment