KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO AITAKA TARI KUSITISHA MAJARIBIO YA GMO.
Mwambawahabari
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew
Mtigumwe leo tarehe 21 Novemba 2018 ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa kilimo
Tanzania (TARI) kusitisha mara moja utafiti na majaribio ya uhandisijeni
(Genetic Modified Organism-GMO) yanayofanyika kwenye vituo vyake vya utafiti.
Aidha, Katibu Mkuu ameilekeza Taasisi hiyo ya TARI
kuwa mabaki yote ya majaribio ya Uhandisijeni yateketezwe mara moja.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Taasisi hiyo kuanza
kutoa matokeo ya utafiti bila kupata idhini ya serikali.
Siku za hivi karibuni Taasisi ya Utafiti wa kilimo
Tanzania (TARI) kupitia kituo cha Makutupora imekuwa inaalika watu mbalimbali
kwenda kuona matokeo ya utafiti wakati serikali haijaruhusu matumizi ya
uhandisijeni nchini.
Post a Comment