SERIKALI YAIPA NFRA BIL 15 UNUNUZI WA NAFAKA ILI KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA CHAKULA YANAPOTOKEA MAJANGA
Mwambawahabari
Waziri
wa Kilimo Dkt Charles Tizeba (Mb), akisisitiza mpango wa serikali
kukabiliana na njaa wakati akihutubia wananchi waliojitokeza
kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani Kitaifa ambayo
yamefanyika kwenye viwanja vya JK Nyerere katika Halmashauri ya Mji wa
Tunduma jana tarehe 16 Octoba 2018. (Picha Na Mathias Canal, WK)
Waziri
wa Kilimo Dkt Charles Tizeba (Mb), akikagua banda la Bima ya mazao
wakati wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani
Kitaifa ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya JK Nyerere katika
Halmashauri ya Mji wa Tunduma jana tarehe 16 Octoba 2018.
Na Mathias Canal-WK, Tunduma-Mbeya
Katika
kukabiliana na upungufu wa chakula unaoweza kujitokeza pindi nchi
itakapokuwa kwenye majanga, Serikali imetoa jumla ya shilingi Billioni
15.0 za Kitanzania kwa ajili ya ununuzi wa mahindi kupitia Wakala wa
Taifa wa Hifadhi Chakula (NFRA) katika mwaka wa fedha 2018/2019.
Tayari Wakala
wa Taifa wa Hifadhi Chakula (NFRA) umeanza msimu wa ununuzi tangu mwezi
Agosti 2018 ambapo nafaka wanayonunua ni kutoka kwa wakulima na vikundi
vya wakulima kote nchini.
Waziri
wa Kilimo Dkt Charles Tizeba (Mb), amebainisha hayo jana tarehe 16
Octoba 2018 wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye kilele cha
maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani Kitaifa ambayo yamefanyika kwenye
viwanja vya JK Nyerere katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma.
Vilevile,
NFRA inaendelea kuboresha uwezo wake wa kuhifadhi nafaka kwa kuimarisha
kanda zake kupitia mradi wa ujenzi wa vihenge na maghala ya kisasa ili
Kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka.
Dkt
Tizeba alisema kuwa Kupitia mradi huo miundo mbinu ya kisasa ya hifadhi
ya chakula zikiwemo maghala na vihenge vya kisasa vinajengwa katika
Halmashauri za Wilaya za Babati (Tani 40,000), Mpanda (Tani 25,000) ,
Sumbawanga (Tani 40,000), Mbozi (Tani 20,000), Songea (Tani 50,000),
Shinyanga (Tani 35,000), Dodoma (Tani 20,000) na Makambako (Tani
30,000).
Alisema,
Hifadhi hizo zitatumia teknolojia ya kisasa ya kuhifadhi mazao na hivyo
kupunguza upotevu wa mazao ghalani kwa kiasi kikubwa.
Aliongeza
kuwa, Kukamilika kwa mradi huo kutawezesha NFRA kuongeza uwezo wake wa
kuhifadhi nafaka kutoka Tani 251,000 hadi kufikia Tani 501,000 ifikapo
mwaka 2019/2020.
Post a Comment