Ads

_NDUGU MOHAMED AWADHI MJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM TAIFA AJA KIVINGINE_. KUSAIDIA MAKUNDI YA VIJANA AANZA NA KUNDI LA WABEBA MIZIGO




Mjumbe wa mkutano mkuuu ccm Taifa kupitia kundi la vijana amekutana na vijana wabeba mizigo wa stendi ya mbezi ijulikanayo kama Police ya Zamani na kuzungumza nao maswala ya kimaendeleo. Hiii ni baada ya ndugu Mohamed Awadhi kuona ipo haja yeye kama kiongozi kuona kundi hilo la vijana ambao ni nguvu ya taifa wakifanya kazi yao hio kwa muda mrefu pasina mafanikio yanayo tia faraja kwa vijana hao na Familia zao jambo ambalo limemshawish ndugu Mohamed Awadhi kukutana nao na kuzungumza nao.

Aidha wakati wanaendelea. Na kikao ndugu Mohamed Awadhi aliwaambia vijana hao Taifa hili lina wategemea sana na wao ndio mashine ya kuharakisha maendeleo ya Nchi hiii na familia zao hivyo yeye kama kijana mwenzao hayupo Tayari kuwaona wakikosa faraja wakipoteza matumaini kwa kukosa mshauri na mtu wa kuwasaidia katika majambo yao ya kimaendeleo na kutatua changamoto wanazo kabiliana nazo pindi wanapo Fanya kazi zao za ubebaji wa mizigo inayo shushwa na gari za mikoani,

Ndugu Mohamed Awadhi aliwaambia kuwa yupo tayari kusaidizana nao kwani faraja yake ni kuona makundi ya vijana yanapata chachu ya maendeleo

Hata hivyo katika kikao chao hicho cha kwanza ndugu Mohamed Awadhi aliwataka vijana hao waanze kujiwekezea shilingi 2000kwa kila mmoja kila siku ambapo kundi la vijana hao wapo 45 ila vijana 30 wakaonekana kukunwa na hoja ile na ndugu Mohamed Awadhi mjumbe wa mkutano mkuu akatoa ufafanuzi wa nini kifanyike kwenye video hapo chini👇🏼👇🏼👇🏼

Hata hivyo mbali na mchanganuo alio utoa ndugu Mohamed Awadhi alihakikisha vijana hao wanapata uongozi utakao shirikiana naye kwenye maswala yao ya kimaendeleo na kisha kuwaasa waandae katiba ili wasajili kikundi chao ili waipate ithibati na kutambulika ili iwe rahisi kwao kukopesheka na kupata ulinzi wa maeneo yao.

Aidha ndugu Mohamed Awadhi hakuacha kuwaweka wazi kuwa ni chama chamapinduzi pekee ndio kina hangaika na shida zao hivyo wasikubali kulaghaika na waanze kuwakataaa wana siasa wasio na dhamira Safi na dira ya maisha yao na maendeleo yao.

Ndugu Mohamed Awadhi mjumbe wa mkutano mkuu Ccm amesema huu ni mwanzo tuu ataendelea kutembelea makundi mengine na kuzungumza nayo ili kubaini changamoto za makundi hayo ili kusaidiana kutatua changamoto hizo.

Mohamed Awadhi
0719969023/0762890656
_*Tukutane kazini*

No comments