MATUKIO KATIKA PICHA WAZIRI MKUU MAJALIWA AKIWA ZIARA WILAYANI BAHI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka katika moja kati ya nyumba
sita za walimu alizozikagua katika Shule ya Sekondari ya Mpalanga
wilayani Bahi, Oktoba 19, 2019. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bahi,
Mwanahamisi Athumani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi baada ya
kukagua ujenzi wa nyumba sita za walimu katika shule ya Sekondari ya
Mpalanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua daraja la Chipanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Bilinith Mahenge, Wanne kushoto ni Mbunge wa Bahi, Omary Badwel na wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Athumani. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua daraja la Chipanga
wilayani Bahi, Oktoba 19, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo na wapili
kushoto ni Mbunge wa Bahi, Omary Badwel. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mganga
Mkuu wa Kituo cha Afya cha Bahi, Kassim Kolowa (kushoto) kuhusu vifaa
vilivyopo kwenye chumba cha upasuaji cha Kituo hicho wakati
alipokitembelea, Oktoba 19, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya
Bahi, Mwanahamisi Athumani. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bibi Subi Mchome, ambaye ni mmoja wa wazazi waliojifungua salama katika wodi ya wazazi ya Kituo cha Afya cha Bahi mkoani Dodoma, Oktoba 19, 2018. Wapili kushoto ni Mganga Mkuu wa Kituo hicho, Kassim Kolowa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mtalaam wa Maabara,
Petronila Olomi (kushoto) wakati alipotembealea Maabara ya Kituo cha
Afya cha Bahi mkoani Dodoma, Oktoba 19, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ,
Selemani Jafo na Wapili kushoto ni Mganga Mkuu wa Kituo hicho,
Kassim Kolowa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wagonjwa wa nje
wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Bahi mkoani Dodoma, Oktoba 19,
2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Post a Comment