MAAFISA AFYA WATAKIWA KUSIMAMIA USAFI WA MAZINGIRA ILI KUTOKOMEZA MALARIA
Na WAMJW – Dar Es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee
na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewaagiza Maafisa Afya nchini kusimamia
kwa ukamilifu usafi wa mazingira katika jamii ili kutokomeza ugonjwa
wa Malaria.
Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo Oktoba 22, 2018
wakati akizindua Taarifa ya Utafiti wa Viashiria vya Ugonjwa wa Malaria
wa Mwaka 2017 katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar Es Salaam.
“Nawaagiza Maafisa Afya, badala ya kupoteza muda
mwingi wa kukagua migahawa, bucha za nyama na sehemu ambazo wanajua
zinaleta fedha, tunataka pia wajikite katika kusimamia usafi wa mazingira
katika Kata, Vijiji na Mitaa yetu”Alisema Mhe. Ummy.
Katika kuhakikisha hali ya usafi wa mazingira inakuwa
endelevu, Waziri Ummy ameagiza Mabalaza yote ya Halmashauri nchini kuweka
Sheria na adhabu kali kwa wote ambao wamekuwa wagumu katika kushiriki
katika usafi wa mazingira huku Waganga Wakuu wa Halmashauri zote nchini
kuhakikisha wanasimamia vyema utekelezaji wa kanuni na sheria za afya
na usafi wa mazingira jambo ambalo litaibua chachu ya ushindi katika
mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria.
“Niyatake Mabalaza ya Hamashauri kuweka hatua kali,
sheria kali na adhabu kali kwa wote ambao hawashiriki katika usafi wa
mazingira” alisema Waziri Ummy.
Licha ya hivyo Waziri Ummy alisema kuwa Serikali
kupitia Wizara inaendelea kutekeleza Mpango endelevu wa ugawaji vya
ndarua kupitia wanafunzi wa shule za msingi, kupitia Kliniki za wajawazito
na watoto, ambayo hujulikana kama Chandarua Kliniki huku hadi sasa jumla
ya vyandarua milioni 31 vimeshagawiwa nchini kote.
Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa Matokeo ya mpango
endele u wa ugawaji wa vyandarua yameonesha kuwa asilimia 78 ya kaya
nchini Tanzania zinamiliki angalau chandarua kimoja chenye dawa, Katika
utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa mwaka
2015-16, ni asilimia 66 tu za kaya zilikuwa zinamiliki angalau chandarua
kimoja chenye dawa huku Umiliki wa vyandarua vyenye dawa ni wa kiwango
cha juu kwa kaya za mijini (asilimia 81) ikilinganishwa na kaya za vijijini
(asilimia 77).
Kwa upande mwingine Waziri Ummy alitaja Halmashauri
zenye maambukizi ya kiwango cha juu ni pamoja na Kakonko 30.8%, Kasulu
DC 27.6%, Kibondo DC 25.8%, Uvinza 25.4%, Kigoma DC 25.1%, Buhigwe 24%,
Geita DC 22.4%, Nanyamba TC 19.5%, Muleba DC 19.4%, Mtwara DC 19.1%,
huku Halmashauri zenye maambukizi ya kiwango cha chini ya asilimia 0.1
ni Mbulu TC, Mbulu DC, Hanang, Hai, Siha, Moshi MC, Mwanga, Kondoa TC,
Meru DC, Arusha CC, Arusha DC, Munduli, Ngorongoro, Rombo DC
Post a Comment