KATIBU TAWALA KIGAMBONI AGAWA HUNDI ZA MIKOPO YA AKINA MAMA,SOMA HAPA YAJAYO YANAFURAHISHA.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando, akigawa hundi kwa vikundi vya
akinama wanaokpeshwa na Manispaa ya Kigamboni mikopo isiyo na riba jumla ya
vikundi 25 leo vimepewa hundi .(Picha na John Luhende)
N a .John
Luhende
Mwamba wa habari
Halmashauri
ya manispaa ya Kigambo leo imeanza kutoa Mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya
akina mama, ambapo vikundi 23 vilivyo
kidhi vigezo vimepatiwa mkopo wenye thamani ya shilingi million 45 bila riba.
Akizungumza
kataika hafla ya kugawa hundi kwa vikundi hivyo vya akinamama Katibu tawala wa
Wilaya ya Kigamboni Raheli Mhando amevitaka
vikundihivo kuzitumiafedha hizo
katika kuendeleza biashara zao na
kuzingatia muda wa kurejesha ili ili waweze kuongezewa zaidi.
‘’Wilaya
yetu bado ni changa tutaendelea kuongeza fedha zaidi kadiri ya uwezo wa Manispaa yetu, naomba
mjitahidi kurejesha kwa wakati na mkikwama msikae kimya mje kutoa taarifa
hatuwezi kuajakuuza vitu vyenu tutawaelewa tunaweza kuwaongezea muda Serikali
yenu sikivu ina wajali‘’alisema
Aidha
Mhando amesema pamoja na kuanza kutoa mikopo hiyo kwa akina
mama,halmashauri inatoa mikopo kwa vijana na walevu ambapo inaendelea kufanyiakazi taarifa za vikundi 18
vyavijana ambavyo vina tarajiwa kukopeshwa Pikipiki.
’’Waambieni
huko na ndugu zetu walemavu waje kuchukua mikopo kwasasa idara inaendelea
kufanyia kazi maelekezo ya mkuu wa Wilaya kwamba mikopo ya pikipiki itolewe kwa
vikundi na siyo kwa mtu mmoja ikikamilika vija nao watapewa Pikipiki “ alisema
Naye Afisa Maendeleo wa Manispaa ya Kigamboni Said
Bakari , amesema Fedha hizo zitaendelea kutolewa kama serikali ilivyo agiza ,ambapo
agizo la Serikali ni kutoa asilimia kumi
ya mapato kwa mgawanyo wa asilimia 4% vijana asilimia 4 %vijana na asilimia 2%
kwa walemavu na sasa ni sheria na wataendelea kuitekeleza.
Kwaupande
wao wanawake walipewa hudi hizo wameishukuru serikali ya awamu yatano kwa
utaratibumzuri wa kuwakopesha lakini wameomba kiasi cha mkopo huo kiweze
kuongezwa pindi wanapo kamilisha marejesho.
‘’Tuna
shukuru Manispaa yetu kwa mikopo hii, itatusaidia sana sisi akinamama na biashara zetu tutajitahidi kurejesha kwa wakati ili tupewe
zaidi na ninawaomba akimama wenzangu
tujitahidi kurejesha .













Post a Comment