Ads

DC Mjema aagiza Takukuru kuwachukulia hatua wafanyabiashara wauza maeneo


Mwambawahabari
Na Heri Shaaban
MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameagiza Maofisa wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa TAKUKURU Ilala kufanya uchunguzi kwa wafanyabiashara wanaouza maeneo ya biashara  Kata ya Kariakoo  na vipande vya barabara.


Mjema aliyasema hayo katika ziara yake ya Kata ya Kariakoo Dar es saalam inayosikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi wake.


"Nakuagiza Ofisa TAKUKURU  Ilala kuanzia sasa anza uchunguzi kwa wafanyabiabiashara wanaouza vipande vya barabara  "alisema Mjema.



Mjema alitoa tamko hilo kufuatia kupokea kero za wafanyabiashara ambao wapo katika orodha lakini wamekosa vizimba vya meza za biashara.

Aidha alimwagiza ofisa Biashara wa Manispaa ya Ilala wagawe upya meza za biashara za Mtaa wa Kongo Kariakoo kufuatia   meza hizo kukodishwa kwa watu wengine ambao sio walengwa.

Alisema zoezi hilo la kugawa upya meza za Wamachinga Kariakoo  litaanza Octobar 26 mwaka huu ambapo amemwagiza Ofisa Masoko kuanza taratibu .


 Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala anazindua miradi ya Maendeleo  na kufanya utatuzi wa kero za wananchi ambapo Mkuu wa Wilaya huyo ameongozana na wataalam mbalimbali na wakuu wa Idara.



No comments