CDF YAFANYA KONGAMANO KUBWA LA SAUTI ZA WASICHANA JIJINI DAR ES SALAAM
Mimba, Ndoa za
utotoni na Ukeketaji bado changamoto kubwa sana kwa taifa, hivyo serikali tunaiomba
kushirikiana na asasi za kiraia kutokomeza mambo haya ikiwa ni pamoja na
kubadilisha sharia ya mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka 18.
Baadhi ya wasichana kutoka mikoa mbalimbali ya hapa nchini wakifuatilia Kongamano kwa umakini.
Hayo yamebainishwa
mapema leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa
Mtoto (CDF) Bw. Koshuma Mtengeti kwenye Kongamano la Sauti ya Wasichana lililofanyika
kwenye chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es salaam (DUCE) huku waandaaji wakiwa ni
CDF.
Kongamano hilo
la siku mbili lililoandaliwa na Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) kwa kushirikiana
na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es
salaam (DUCE) chini ya ufadhili wa shirika la FORWARD UK na Ubalozi wa Uswidi
Tanzania, na kuwakutanisha wasichana zaidi ya 150 kutoka mikoa ya Mara, Dodoma,
Mwanza na Dar es salaam.
Mkurugenzi
huyo alisema kuwa lengo kuu la kongamano hilo ni kuwajengea uwezo watoto wa
kike kuweza kujitambua na kutambua haki zao pamoja na kuchukua hatua stahiki
pale ambapo haki zao zinavunjwa.
Aliongezea
kuwa Ukeketaji bado ni kitendo kinachozidi kuchukua nafasi kubwa hapa nchini, Na
kusema kuwa mwaka huu ni msimu wa ukeketaji na baadhi ya maeneo watoto
wameshaanza kukeketwa, hivyo sisi kama watetezi wa watoto hawa tunahitaji kuona
serikali inachukua hatua stahiki juu ya watekelezaji wa vitendo hivi.
Aidha kongamano
hilo litawahusisha wadau wa mtoto wa kike pamoja na washirika wa CDF kwenye
mradi wa binti ambao ni UMATI na Wadada Centre, lakini pia kongamano hilo
litakuwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani kwa mwaka 2018 yenye kauli mbiu isemayo
“Imarisha
uwezo wa mtoto wa kike tokomeza Ukeketaji, Mimba na Ndoa za Utotoni”
Kwa upande
wake DR. Ikupa alisema kuwa wao DUCE wananafasi kubwa ya kuwatengeneza walimu
ambao ndio wanaenda kuwalea watoto huko mashuleni na huko watakutana na watoto
mchanganyiko ambao wengine wametoka katika mila kandamizi na maeneo mengine
mengi.
Aliendelea kusema
kuwa chuo chao kimeshirikiana ipasavyo na CDF katika kuhakikisha wanawajengea
uwezo watoto wa kike hawa ili waweze kujiamini, kujitambua, na kuweza kupambana
kushiriki katika nafasi mbalimbali za kiserikali, Kiuchumi na ukombozi wa
mwanamke.
Mkurugenzi Mtendaji wa (CDF) Bw. Koshuma Mtengeti akiongea na waandishi wa habari mapeama leo jijini Dar es salaam katika Kongamano la Siku ya Wasichana 2018.
Mkurugenzi Mtendaji wa FOWARD UK, Naana Otoo Oyorfey akiongea na wasichana waliofika katika kongamano hilo.
Mratibu wa kitengo cha jinsia kutoka Chuo Kikuu cha (DUCE) Dk. Ikupa Moses Ndambo akitoa ufafanuzi wa jambo mapema leo jijini Dar es salaam.
Washiriki wakifuatilia kwa makini Kongamano la Sauti za Wasichana 2018.
Washiriki wakicheza burudani ya muziki.


Post a Comment