CCM ILALA WAMUENEZI MWALIMU NYERERE KWA MATEMBEZI, NA KUFANYA USAFI NYUMBA ALIYOISHI.
Na. John Luhende
Mwambawahabari
Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala katika kumuenzi hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo kimefanya matembezi ya Kilomita tatu yaliyoishia katika shule Sekondari Pugu .
’’Watanzania tukimuiga na kumuishi mwalimun kama anavyofanya Rais wetu Dr John Pombe Magufuli nchi yetu itapigahatua kimaendeleo nawaomba watanzania na wanana ccm tumuenzi mwalimu kwa vitendo” alisema
Kwaupande wake katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Joyce Ibrahimu Mkaugala,amasema wanaIlala wamejitolea katika matembezi na kufanya usafi katika juma zima na wameonyesgha moyo wa umoja katika kumuenzi Mwalimu haya yote nikunesha kuwa Mwalimu alikuwa ni kiangozi wa mfano.
“Mwalimu alitaka kila mtu awajibike afanye kazi alikemea sana uvivi akiaminin kuwa kazi ndiyo njia pekee ambayo inaweza kuleta maendeleo pia alikemea ubaguzi wa rangi na ukabila na sisi hapa tuna sisitiza sote tuwe na ummoja”alisema
Naye mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo Angelo Lwiza amewataka watanzania kumuenzi mwalimu Nyerere hasa katika nyumba alizoishi kuwekwevitabu alivyo vitunga na kuviandika mwalimu ili iwe kumbukumbu kwa vizazi vijavyo












Post a Comment